May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo wa Polisi afariki dunia

Spread the love

DHAHIR Kidavashari (56), Aliyekuwa kaimu Kamishna wa fedha na lojistiki wa Jeshi la Polisi Tanzania amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 17 Novemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa kutoka kwenye familia yake zinaeleza, Kadavashiri alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya DCMC Ntyuka iliyopo jijini humo, na kwamba alifikishwa kwenye hospitali hiyo tarehe 15 Novemba 2020.

David Misime, msemaji wa jeshi hilo ameeleza kwamba, mwili wa Kidavashiri utaagwa tarehe 18 Novemba 2020 katika eneo la Kisasa, na baada ya hapo utapelekwa Arusha kwa taratibu zingine za mazishi.

Wakati wa uhai wake, akiwa ziarani mkoani Kagera tarehe 21 Agosti 2020, kuangalia utayari wa jeshi hilo kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu, Kidavashari aliwaonya wanasiasa wanaotaka kufanya fujo kuwa watachukuliwa hatua.

Alisema, polisi wako tayari kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani huku akiwafananisha wale wantakaofanya vurugu kama wateja wao ambao watawahudumia.

“Sisi tuko tayari kwa yoyote atakayefuata sheria na taratibu, lakini kuna wateja ambao tutawapata, sisi kwetu mteja ni mfalme, tutampa kulingana na huduma anayoitaka.”

“Ukikiuka sheria, tutampa huduma anayotaka, ni vyema ukatii sheria bila shuruti. Watii sheria bila kushurutishwa ili twende kwenye uchaguzi na kumaliza kwa amani, usichokoze polisi kwani tuko tayari kuwahudumia kadri watakavyoomba,” alisema Kidavasharia aliyekuwa

 

error: Content is protected !!