March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo wa Acacia kizimbani kwa utakatishaji fedha

Spread the love

ASA Mwaipopo (55), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za Madini za Bulyanhulu, North Mara na Pangea zilizokuwa chini ya Acacia, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashtaka tisa yanayomkabili ikiwemo utakatishaji fedha na kughushi, na kujipatia dola za marekani 840,000. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mwaipopo amesomewa mashtaka hayo leo tarehe 23 Oktoba 2018 na Mawakili wa Serikali, Faraja Nchimbi na Jacqline Nyantori mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Upande wa mashtaka umedai kuwa, Mwaipopo ametenda makosa hayo ya kula njama, kuongoza uhalifu wa kupangwa, kughushi, ukwepaji kodi na utakatishaji fedha, katika kipindi cha Aprili 11 mwaka 2018 na Juni 30 mwaka 2017.

Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 31 Oktoba 2018 kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi.

error: Content is protected !!