May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo PPRA afariki dunia

Spread the love

 

AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leonard Kapongo, amefariki dunia jioni ya jana, tarehe 17 Julai 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarufa hiyo imetolewa leo tarehe 18 Julai 2021 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPRA, Dk. Matern Lumbanga.

Taarifa ya Dk. Lumbanga imesema, Marehemu Mhandisi Kapongo amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, aliokuwa anapatiwa matibabu.

“Kwa sasa ofisi inawasiliana na kushirikiana kwa karibu na familia ya marehemu kwa taratibu za mazishi. Tunatoa pole kwa familia ya marehemu, waday wa ununuzi wa umma na wahandusu iwa kuondokewa na mpendwa wetu,” imesema taarifa ya Dk. Lumbanga.

Taarifa hiyo imesema, taratibu za mazishi zitatolewa baadae.

Mhandisi Kapongo ameitumikia mamlaka hiyo tangu tarehe 26 Oktoba 2018, alipoteuliwa na Hayati John Magufuli, kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, hadi umauti ulipomkuta jana.

error: Content is protected !!