September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo CUF yamemkuta, asimamishwa

Spread the love

BARAZA Kuu la Uongozi la Chama Cha Wananchi (CUF) limetangaza kumsimamisha uongozi, Makamu Mwenyekiti wake Zanzibar, Abbas Juma Muhunzi kwa kukiuka Maadili ya Uongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Uamuzi huo umefikiwa jana Jumapili tarehe 28 Juni 2020 katika kikao cha Baraza hilo lililokutana jijini Dar es Salaam.

Muhunzi amekutana na kibano hiko miezi kadhaa kupita tangu waliokuwa viongozi waandamizi wa CUF kutimikia ACT-Wazalendo akiwemo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Maalim Seif aliyekuwa katibu mkuu aliondoka huku wanachama na viongozi wengi upande wa Zanzibar huku Muhunzi akisalia CUF.

Kusimamishwa kwake, kumeelezwa na
Mohamed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kupitia taarifa kwa umma.

Amesema, baada ya wajumbe kupokea tuhuma dhidi ya Muhunzi na kufanya mjadala wa kina, baraza hilo lilitoa nafasi kwa mlalamikiwa kujitetea.

Ngulangwa alisema makosa yaliyowasilishwa na wajumbe dhidi ya Muhunzi kwa kuzingatia Ibara za (83)(1)(b) na 94(1) na 94(2) zinazolipa mamlaka Baraza la Uongozi kushughulikia makosa ya viongozi wakuu.

“Muhunzi alikiri kufanya makosa yaliyoelekezwa kwake na akakiachia kikao kuamua dhidi yake.”

“Wajumbe waliamua kupiga kura ya kumsimamisha uongozi ambapo wajumbe 42 walitaka Muhunzi asimamishwe, saba walipinga kusimamisha na sita hawakuunga mkono wala kupinga,” inaeleza taarifa hiyo

Licha ya kutoelezwa hasa makosa aliyoyafanya, Ngulangwa alisema,”Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, maamuzi ya kumsimamisha Muhunzi yanaatahili kufikishwa kwenye mkutano mkuu kwa maamuzi ya mwisho ndani ya siku 90 kuanzia leo.”

error: Content is protected !!