December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo CCM aivua nguo UVCCM

Kheri James, Mkuu wilaya ya Ubungo

Spread the love

KAPTENI Mstaafu, Alhaji Mohammed Ligora aliyewahi kuwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, amewashukia makada wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kwa kushindwa kuibua masuala ya ufisadi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya uchambuzi wa miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, Alhaji Ligora amesema ni aibu kwa mkuu wa nchi kuibua ufisadi huku vijana hao wakikaa kimya. 

Alhaji Ligora ameeleza kuwa, kitendo cha Rais Magufuli kuibua ufisadi katika mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, wakati umoja huo ukishindwa kupaza sauti, kinatia aibu.

“Mko vijana wengi wasomi Dar es Salaam, Vinguguti kuna mabilioni ya fedha yalitengwa kwa ajili ya kujenga machinjio. Lakini iko wapi machinjio?” amehoji Alhaji Ligola na kuongeza.

“Rais Magufuli alikwenda akakuta ubadhirifu, mlikua wapi hadi Rais anaenda. Niwakumbushe haiwezekani kuwepo ubadhirifu halafu wana UVCCM wasipaze sauti zao.”

Alhaji Ligora amewashauri vijana wa UVCCM kuiga mfano wa vijana wa enzi za TANU ambao walikuwa bega kwa bega na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kupigania uhuru na maendeleo ya Taifa.

Deus Lugaila, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Sauti ya Jamii, amesema taasisi hiyo inampongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake katika kupambana na rushwa nchini.

Lugaila amesema taasisi yake imeandaa uchambuzi wa miaka minne ya utendaji wa serikali iliyoko madarakani, kwa ajili ya kuufahamisha umma wa Tanzania, mambo aliyofanya Rais Magufuli.

“Miongoni mwa mambo hayo ni uboreshaji wa utendaji wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kwa kununuaji ndege, uboreshaji miundombinu kama barabara, elimu bure, madawati, hodsitali za wilaya na kudhibiti mianya ya rushwa na kurudisha heshima kwa watumishi wa umma,” amesema Lugaila.

error: Content is protected !!