August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo Bavicha mbaroni kwa tuhuma za makosa mtandao

Mratibu wa uhamasishaji wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya

Spread the love

 

MRATIBU wa uhamasishaji wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya, anadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, kwa tuhuma za makosa ya kimtandao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya tukio hilo imetolewa leo Ijumaa, Julai Mosi, 2022 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Bavicha, Apolinary Boniface.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mwaipaya amekamatwa jana tarehe 30 Juni 2022, mkoani Morogoro na kwamba leo asubuhi amesafirishwa kuelekea mkoani Dodoma, anakodaiwa kutekeleza makosa hayo.

“Bavicha tunalitaka Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kumweleza Mwaipaya kosa analotuhumiwa nalo na kumwachia huru au kumpa dhamana kwa kuwa kosa wanalodai kumtuhumu nalo lina dhamana,” imesema taarifa ya Boniface.

MwanaHALISI Online ilipomtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuthibitisha taarifa hizo, simu yake iliita bila kupokewa. Jitihada za kumpata zinaendelea.

error: Content is protected !!