Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kigogo ATCL aliyeisababishia Serikali hasara Bil. 71 ahukumiwa faini Mil. 8
Habari Mchanganyiko

Kigogo ATCL aliyeisababishia Serikali hasara Bil. 71 ahukumiwa faini Mil. 8

Spread the love

 

ALIYEKUA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela, au faini ya Sh. 8 milioni, baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. 71 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Washtakiwa wenzake katika kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka iliyokuwa na mashtaka sita, ni aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk. Ramadhan Mlinga na aliyekuwa Mwanasheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka.

Washtakiwa hao wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, au faini ya Sh. 2 milioni kila mmoja.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega.

Katika kesi hiyo, Mattaka alishtakiwa kutenda kosa hilo tarehe 9 Oktoba 2007, alipokuwa Mkurugenzi Mkuu ATCL.

Akidaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air Bus, ambao umeiingizia hasara Serikali ya zaidi ya Sh. 71 bilioni.

Mattaka alidaiwa kusaini mkataba huo kwa ajili ya kukodisha ndege , bila ya kuwa na kibali cha Serikali. Mkataba huo alisaini na Kampuni ya Wallis Trading Inc.

Kwa upande wa wenzake, wanadaiwa tarehe 19 Machi 2008, kwenye Ofisi za PPRA, zilizoko Ilala jijini Dar es Salaam, walighushi   muhtasari wa kikao cha mamlaka hiyo, ulioonesha maombi ya ATCL ya kukodisha ndege yameidhishishwa.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi zaidi ya 20, akiwemo aliyekuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Yamungu Kayandabila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!