September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kigamboni kujenga kituo cha polisi

Spread the love

WILAYA mpya ya Kigamboni imeanza mkakati wa kujenga vituo vya polisi ili kushughulikia wavuvi pamoja na wahamiaji haramu, anaandika Regina Mkonde.

Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya Kigamboni amesema kuwa alipata taarifa kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwamba wilaya yake ndiyo njia ya wahalifu hao.

Mgandilwa alikuwa akishiriki zoezi la usafi lililoshirikisha wakazi wa wilaya hiyo,

“Nilipata taarifa kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kuwa wilaya yangu ndio njia ya wahamiaji haramu, ndipo nikafanya maamuzi ya ujenzi wa vituo vya polisi kwenye wilaya yangu,” amesema na kuongeza.

“Mkakati wangu kwa sasa ni kuimarisha ulinzi na usalama, kupambana na wavuvi haramu kwa kuanzia nitajenga vituo viwili ikiwemo cha Pemba Mnazi. Hadi sasa nina rasilimali za ujenzi wa vituo viwili vya polisi.”

Amesema kutokana na wilaya hiyo kuwa mpya, changamoto zilizopo ni nyingi na kwamba kuna mikakati aliyoweka ili kuziondoa wakati muafaka utakapofika.

“Kuna changamoto nyingi na mikakati yake ipo imeshawekwa lakini kwa sasa nahangaikia uanzishwaji wa manispaa na mikakati mingine itwawekwa wazi muda utakapofika,” amesema.

Kuhusu zoezi la usafi, Mgandilwa amewataka wafanyabiashara kuweka vyombo vya kuhifadhia uchafu, pamoja na wananchi kutotupa taka ufukweni kwa kuwa kitendo hicho kitaifanya fukwe kuwa kama choo.

“Kwa mtu atakaye toa taarifa ya mtu anayetupa taka ufukweni nitatoa kiasi cha fedha kumzawadia,” amesema

 

 

error: Content is protected !!