January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigaila ampinga Mavunde Dodoma

Spread the love

MGOMBEA Ubunge katika jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila amekata rufaa ya kupinga uteuzi wa mgombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Anthon Mavunde. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akuzungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kigaila amesema awali aliweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea huyo kutokana na kutokuwa na sifa za kugombea nafasi hiyo.

“Mgombea huyo hana sifa za kumfanya ateuliwe kugombea nafasi hiyo kwa sababu amekiuka taratibu na kanuni za utumishi wa Umma akiwa yeye mtumishi wa Umma.

“Kwenye fomu yake ya uteuzi kifungu (5) amekiri kuwa yeye bado ni mtumishi wa Umma kwa ngazi ya Mkuu wa Wilaya hivyo Mavuinde hadi anarudisha fomu za Tume 21 Agosti mwaka huu bado alikuwa mkuu wa wilaya jambo ambalo ni kinyume na waraka wa maadili ya utumishi wa Umma.

“Mbali na hilo inaonesha wazi kwamba Mavunde ambaye ni mkuu wa wilaya bado analipwa mshahara na kodi za watanzania wenye vyama na wasiokuwa na vyama,” amesema Kigaila.

Alisema kwa mujibu wa Mavunde jinsi alivyojaza fomu ya tume yeye bado ni mkuu wa wilaya na hivyo amekiuka sheria na kuudanganya umma na kukiuka kiapo hivyo hastahili kuwa mgombea.

Hata hivyo Kigaila amesema kutokana na pingamizi hilo alipokea majibu kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma akidai kuwa pingamizi hilo amelitupilia mbali kwa sababu maelezo yake yanahusu watumishi wa umma.

“Nilijibiwa kuwa, kwa mujibu wa waraka wa Rais Na.1 wa Mwaka 2015, 7 Julai, mwaka huu alitoa utaratibu utakaotumika kwa Mawaziri, Naibu waziri, Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya watakaoamuya kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, kwa mgombea ataketeuliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi likizo yake itaendelea hadi Tume itakapotangaza matokeo,” amesema Kigaila.

Alisema aliambatanishiwa na barua ya ruhusa ya Mavunde ya kuanzia 11 hadi 22 Agosti, mwaka huu na hiyo siyo fomu ya likizo kwa kuwa mgombea huyo ana muda wa miezi miwili tangu ateuliwe kushika wadhifa wa ukuu wa wilaya na taratibu za utumishi wa umma hapaswi kwenda likizo bali anapaswa kupewa ruhusa hivyo mgombea Mavunde anaruhusiwa kuendelea na mchakato wa ubunge wa jimbo hilo.

Alisema alifika hatua hiyo ya kukata rufaa kutokana na mgombea huyo kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 pamoja na marekebisho yake, waraka wa utumishi wa umma na waraka wa Rais.

“Ndugu Mavunde hajaacha kazi wala kuchukua likizo hadi 21 Agosti mwaka huu siku ambayo Tume ilitakiwa kumteua, na hadi sasa ndugu Mavunde anaomba kugombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini akiwa mtumishi wa Umma (Mkuu wa Wilaya) kinyume na sheria ya uchaguzi, waraka wa utumishi wa Umma na kinyume na waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2015.

error: Content is protected !!