RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amesema, mchango uliotolewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli (61) kwa taifa hilo “hauwezi kusahaulika.” Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Rais Kagame ametumia ukurasa wake wa Twitter, kutoa salamu hizo za rambirambi, kufuatia kifo cha Rais Magufuli, aliyefariki dunia jana Jumatano saa 12:00 jioni, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho, mkoani Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akitangaza msiba huo alisema, Rais Magufuli, alifikwa na mauti wakati akiendelea na matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo.
Rais Kagare amesema “nasikitika kumpoteza kaka na rafiki, Rais Magufuli. Mchango wake kwa nchi yetu hauwezi kusahaulika.”
“Tunatuma salamu za rambirambi kwa familia na wananchi wa Tanzania. Wananchi wa Rwanda wako pamoja na Watanzania katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo,” amesema Rais Kagame
R.I.P
Mheshimiwa rais wetu dk john pombe magufuli umetusaidia sana katika kusoma bure hatimaye tumejua kiingereza
God bless your spirit