July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kifo cha Magufuli, Majaliwa awashukuru wasanii

Spread the love

 

WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewashukuru na kuwapongeza wasanii wote nchini waliojitoa kutunga nyimbo mbali mbali za kumuenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati Dk, John Magufuli. Anaripoti Matilda Peter…(endelea) 

Majaliwa ameyasema hayo hii leo tarehe 22 Machi, 2021 jijini Dodoma katika shughuli ya kitaifa ya kumuaga hayati Magufuli iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Katika hotuba yake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu na waombolezaji wengine, Majaliwa alishukuru kundi hilo la wasanii ambao mara baada ya hotuba hiyo kuisha waliimba wimbo maalumu wa maombolezo kwa alaiki iliyouzulia hapo.

Wasanii walioudhulia na kutumbuiza wimbo huo ni pamoja na Linah, Nandy, Marioo, Khadija kopa, Ben pol, Dogo janja, Jay melody, Stamina, Young Lunya, Goodluck Gosbert na mrisho mpoto.

Toka aliyekuwa makamu wa Rais Samia Suluhu kutangaza kifo cha Magufuli tarehe 17 Machi, 2021 nyimbo Zaidi ya 20 za maombolezo zilitungwa kutoka kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi.

Majaliwa Kassim, Waziri Mkuu wa Tanzania akiaga mwili wa Hayati John Magufuli

Wasanii wengeni walioweza kuimba nyimbo ni pamoja na Harmonize, Rayvany, Rosaree, Nandy, Juma Jux, Shilole, Ommy dimpoz, Peter msechu, Kala jeremiah, One six, Zuchu, Alikiba, Marioo, Darassa, na Mzee yusuph

error: Content is protected !!