MTENDAJI Mkuu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Daniel Loya amefariki dunia asubuhi ya leo Jumatano, katika Hospitali ya Lugalo alikokuwa anapatiwa matibabu.
Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo tarehe 10 Februari 2021 na Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa TCD.
Zitto ametuma salamu za pole kwa familiya ya Loya, na vyama wanachama wa TCD, ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), na ACT-Wazalendo.
“Mtendaji Mkuu wa TCD Bwana D. Loya amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Lugalo.
“Nikiwa Mwenyekiti wa TCD, natoa pole kwa familia ya ndugu Loya na kwa viongozi wote wa vyama wanachama wa TCD, Chadema, CCM, CUF na ACT-Wazalendo,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.
Mwenyekiti huyo wa TCD amesemaTanzania imepoteza mwanademokrasia wa dhati “tumepoteza mwanadekrasia wa dhati.”
Leave a comment