October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kifo cha Floyd: Miji saba taharuki, Trump – Meya washambuliana

Raia wa Marekani wakiandamana kupinga kifo cha Mmarekani mweusi, Goerge Floyd aliyeuwawa na polisi

Spread the love

MIJI saba nchini Marekani inatawaliwa na vurugu na maandamano, ni kutokana na polisi wa Minnesota kufanya mauaji kwa George Floyd, Mmarekani mweuzi. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Maandamano makubwa zaidi yanashuhudiwa katika mji wa Minneapolis na St. Paul, ambayo ipo karibu na hutambulika kama ‘miji pacha.’

Jana tarehe 28 Mei 2020, miji hiyo ndiyo iiyoripotiwa kuwa na maandamano huku waandamanaji wakishutumu polisi kuendesha mauaji hayo kwa mtu asiye na hatia.

Wamarekani weupe kwa weusi wameshikwa na hasira hasa baada ya kushuhudia video iliyomuonesha Floyd akiwaeleza polisi hao ‘msiniue…, nashindwa kupumua,’ licha ya kauli hiyo, Floyd alipuuzwa.

Floyd (46), alikuwa ofisa usalama kwenye mgahawa mmoja Minneapolis. Kijana huyo alikabiliana na mteja mmoja aliyefika mgahawani hapo akijaribu kununua bidhaa kwa kutumia noti bandia ya Dola 20, baada ya polisi kufika eneo hilo, walimgeuzia ‘kibao.’

Rais wa Marekani, Donald Trump

Waandamanaji wanadai hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya polisi walioendesha mauaji hayo. Hata hivyo, waandamani kutoka St. Paul walikutana na upinzani mkali kutoka kwa polisi, sambamba na kumwagiwa maji washa.

Zaidi ya maeneo ya biashara 170 yamefungwa kutokana na vurugu hizo. Waandamani hao walibeba mabango yaliyoandika majina ya Floyd pamoja na wamarekani weusi waliouawa katika siku za karibuni ikiwa ni pamoja na Ahmaud Arbery na Breonna Taylor.

Miji mingine iliyoripotiwa kuwa na vurugu kutokana na mauaji hayo ni Denver, Colorado, Phoenix na Arizona.

Kutokana na taharuki kushika kasi zaidi Minnesota, Donald Trump, Rais wa Marekani amemtuhumu meya wa jiji hilo Jacob Frey kwamba uongozi wake ni dhaifu na kusababisha maandamano hayo kuendelea na kupokewa na miji mingine.

Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter usiku wa kuamkia leo tarehe 29 Mei 2020, “kuna ongozi dhaifu. Jacob Frey ni meya dhaifu kabisa, afanye kazi ipaswavyo na mji urudi kwenye amani vinginevyo nitatuma kikosi kazi.”

Hata hivyo, Meya Frey amejibu twitter usiku huo huo akisema “udhaifu wangu ni kutochukua hatua kwa namna anavyotaka yeye.

“Udhaifu ni kumnyooshea kidole mtu wakati kuna mtikisisko kama huu? Donald Trump hajui chochote kuhusu uimara wa Minneapolis. Tupo imara kabisa. Kwani hiki ni kipindi kigumu zaidi?”

Meya alitembelea maeneo yaliyofanyiwa uharibifu mkubwa na waandamanaji usiku wa kuamkia leo, akisema “tulichokiona masaa machache yaliyopita ni jambo lisilokubwalika. Hatuwezi kuvumilia.”

“Kuna maeneo muhimu mno watu wanayahitaji, kuna banki ambapo watu wanakwenda kuchukua pesa, kuna maduka watu wanaenda kupata chakula na maduka ya madawa watu wanakwenda kupata dawa. Haya ni maeneo muhimu, yanapaswa kulindwa.”

error: Content is protected !!