Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kifo cha Dk. Magufuli: Rais Ndayishimiye amtumia ujumbe Rais Samia
Habari za Siasa

Kifo cha Dk. Magufuli: Rais Ndayishimiye amtumia ujumbe Rais Samia

Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli
Spread the love

 

RAIS wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amemtumia ujumbe Rais waTanzania, Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Magufuli alifariki dunia katika Hospitali ya Mzena, Mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo, na mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, ujumbe huo wa Rais Ndayishimiye, umewasilishwa kwa Rais Samia, leo Ijumaa tarehe 21 Mei 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, na Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Burundi, Ezechiel Nibigira.

Katika ujumbe huo, Rais Ndayishimiye amemhakikishia Rais Samia kwamba Tanzania na Burundi zitaendelea kushrikiana katika masuala ya miundombinu inayounganisha mataifa hayo mawili.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiaga mwili wa Hayati John Magufuli

“Ngibira amesema Rais Ndayishimiye yupo tayari kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano wa Burundi na Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Samia ikiwa ni pamoja na kutekeleza makubaliano ya kuendeleza miundombinu ya usafiri wa reli, barabara, anga na meli inayounganisha nchi hizi mbili,” imeeleza taarifa ya Msigwa.

Aidha, Rais Ndayishimiye amepongeza hatua ya Tanzania kupokea kwa utulivu ugatuaji wa madaraka, kufuatia kifo cha Dk. Magufuli, aliyefia madarakani baada ya kuiongoza nchi kwa miaka mitano mfululizo na miezi mitano (Novemba 2015-Machi 2021).

“Ngibira amesema Rais Ndayishimiye ana matumaini kuwa Tanzania itaendelea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo, chini ya uongozi wa Rais Samia na amepongeza uwepo wa utulivu na mshikamano wa Watanzania katika kipindi chote cha kubadilishana madaraka jambo ambalo ni mfano wa kuigwa,” imesema taarifa ya Msigwa.

Kwa upande wa Rais Samia, taarifa hiyo imesema kiongozi huyo ameahidi kuendeleza ushirkiano wa mataifa hayo mawili.

“Kwa upande wake, Mhe. Rais Samia amepokea salamu za pole na pongezi, na amemhakikishia Mhe. Rais Ndayishimiye kuwa Tanzania itaendelea kuungana na Burundi katika masuala mbalimbali ya uhusiano kama majirani, marafiki na ndugu wa kweli,” imesema taarifa ya Msigwa na kuongeza:

“Amemhakikishia kuwa mambo yote ya makubaliano kati ya nchi hizo ikiwemo miradi ya pamoja kama vile barabara, meli, usafiri wa anga, kituo cha pamoja mpakani na reli itaendelezwa ili kuharakisha maendeleo ya nchi zote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!