Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kifo cha Baloch, Canada katikati ya shinikizo zito
Makala & Uchambuzi

Kifo cha Baloch, Canada katikati ya shinikizo zito

Spread the love

JUSTIN Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada anatakiwa kuchunguza kifo tatanishi cha mwanaharakati Karima Baloch. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Ni kutokana na shinikizo kutoka kwa Baraza la Kimataifa la Haki za Binadamu kumtaka Waziri Trudeau kuunda tume huru kuchunguza kutekwa na kufariki kwa mwanaharakati huyo katika mazingira yanayoacha maswali mengi.

Baloch aliyekuwa kiongozi maarufu wa Jumuiya ya wanafunzi wa Balochistan, alitoroka nchini Pakistan mwaka 2016 na kuingia wenda Canada kama mkimbizi, amekutwa amekufa mbele ya bandari jirani na ufukwe wa Ziwa Toronto.

Baloch, ambaye alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Balochistan,  Pakistan aliuawa kwa siri na watu wasiojulikana jijini Toronto, Canada baada ya kutekwa nyara.

“Sisi watia saini wa rufaa hii, tunamtaka Waziri Mkuu Trudeau kuunda mara moja Tume Huru ya Uchunguzi dhidi ya mauaji ya mwanaharakati huyu wa Baloch kisiwani hapo,” alisema mmoja wa Wanaharakati wa Baraza la Kimataifa la Haki za Binadamu (IHRC) na kuongeza:

“Pia serikari ya Kanada lazima ichunguze uwezekano wa mashirika ya ujasusi ya Pakistan, kama yanahusika katika mauaji hayo.”

Taarifa zinaeleza kuwa,  Baloch alitekwa Jumapili ya tare he 20 Desemba 2020 saa 9 alasiri huku   jeshi la polisi jijini Toronto likiomba msaada kwa umma kutoa taarifa popote atakapopatikana.

Baadaye  polisi walikuta mwili wa Baloch kando ya Ziwa Toronto, katika kisiwa kilichopo jijini humo.

Mwaka 2016, kituo cha habari cha BBC kilimjumuisha Baloch kwenye orodha ya “Wanawake 100 wa BBC 2016.”

Moja ya kazi zake ilikuwa ni kuendesha kampeni za ukombozi wa Balochistan kutoka katika utawala wa Pakistan.

Alikuwa akitumia mitandao ya kijamii kuonesha kukithiri kwa utekaji nyara, mateso, kupotea watu na uvunjifu wa haki zingine za kibinadamu  unaofanywa na Serikali ya Pakistan na jeahi lake dhidi ya Balochistan.

Katika harakati, alitilia mkazo kupigania haki za wanawake wa Balochi na alionesha namna ambavyo vyombo vya sheria na makundi ya kidini Pakistan vinavyoweza kutumia mifumo ya kiserikali,  kijamii kwa dhamira ya kuwakomboa wanawake wanaotoka katika makundi yaliyo hatarini.

Kwa mujibu wa IHRC, Karima aliuawa na mtandao wa mashirika ya ujasusi kwa njia ile ile iliyotumika katika tukio la mauaji ya mwandishi wa habari wa Baloch, Sajid Balochi huko nchini Swiden.

Kabla ya kifo chake, Karima alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kutozwa faini ya kiasi cha Rupia 150,000 sawa na dola 1,875 za Marekani.

Ni baada ya kuwaongoza  mamia ya wanawake katika maandamano dhidi ya vitemdo vya kupotea watu katika mazingira ya kutetanisha Agosti 2006.

Hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo nchini humo, alituhumiwa pia kuondoa bendera bila ruhusa kutoka jengo la serikali kinyume na kifungu cha 123 B cha sheria ya Pakistan.

Karima alitiwa hatiani kwa kosa la kuchafua bendera na uasi, ambapo chini ya kifungu cha 124 A cha sharia ya Pakistan  “Mtu yeyote kwa maneno au ishara au kwa matendo yanayoonekana ataibua chuki dhidi ya serikali ya shirikisho au jimbo, atakuwa ametenda kosa kisheria.”

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya kupambana na ugaidi  huko Turbat, Mkoa wa Balochistan tarehe 2 Juni 2009 nchini Pakistan.

Karima aliliweka moyoni suala la watu kutoweka, alifanya kampeni dhidi ya kutoweka kwa mmoja wa wajomba zake, Abdul Wahid Qamber Baloch.

Wahid ambaye alikamatwa Machi 2007, aliteswa na kushikiliwa kwenye  mahabusu za kijeshi kwa miezi tisa ambapo baadaye  alikabidhiwa kwa polisi Aprili 21  mwaka 2008.

Hata hivyo, Wahid aliashinda makosa tisa kati ya 10 katika kesi yake lakini bado aliendelea kushikiliwa na kushtakiwa kwa shughuli za kupingana na serikali.

Mwingine, Dk. Khalid Baloch, aliuawa  Agosti 2007 kupitia mpango maalum ulioandaliwa, ambapo kikosi cha polisi katika serikali ya kijeshi ya Pakistan, ilidai kuwa ametekwa.

Mwaka 2014 kiongozi mmoja wa jumuiya ya wanafunzi wa Baloch- Awami Zahid Baloch alitiwa mikononi mwa jeshi akiwa katika kikao cha siri, kilichokuwa kikipanga hatua za kuchukua dhidi ya kukithiri kupotea kwa wanafunzi katika mazingira ya kutatanisha.

Ni wakati huo ambapo Karima Baloch aliteuliwa kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo ya wanafunzi wa Baloch.

Baada ya kupewa uongozi huo, mashirika ya kijasusi na vikosi maalumu vya polisi vilianza kumtafuta na kuvamia nyumba za ndugu zake ili kumkamata.

“Kwa kuhofia maisha yake, aliamua kutoroka na kwenda Canada mwaka 2016.

“Hata hivyo, pamoja na kuwa uhamishoni nchini Canada, haikuwa sababu ya kuacha harakati zake za kupigania haki za watu wa Baloch,” alisema Mwanaharakati wa IHRC.

Katika harakati zake, Karima aliwahi kuwasilisha kesi ya kutoweka kwa watu wa Baloch zaidi ya elfu 20 katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Kufuatia kifo chake cha kutatanisha, Waziri wa Mambo ya Bunge nchini humo, Muhammad Ali Khan alitoa orodha ya taasisi za serikali zinazolengwa, huku akiandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa kifo cha Karima ni kizuri sana.

“Kwa  masikitiko  alitamani kuona wanaharakati wengine na wapinzani dhidi ya mamlaka za serikali kama vile Tarek Fateh, na Mwanablogu Goraya na Taha Siddiqui kushughulikiwa,” aliongeza.

Hii si mara ya kwanza kwa maofisa wa serikali kupatikana wakiwa na mipango ya pamoja na jeshi la usalama ya kulenga na kupoteza watu.

Jenerali Pervaiz Musharaf, dikteta wa zamani wa jeshi la Pakistan katika moja ya mahojiano yake na viongozi wa kidini alisema wazi kuwa, wanaharakati na wale wanaothubutu kuinua sauti yao dhidi ya serikali wanapaswa kuuawa popote walipo.

“Sisi tuliosaini hapa tunaitaka serikali ya Canada kusimamia usalama wa wakimbizi wote wa kisiasa nchini humo, kwani wanazidi kuwa katika hatari ya kutoweka kwa kuuawa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & Uchambuzi

Kondomu zinavyotumika kufukuza Tembo

Spread the loveMIKUMI ni miongoni mwa hifadhi za Taifa, inashika nafasi ya...

Makala & Uchambuzi

Ujio wa Kamala Harris: Fahamu uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Marekani

Spread the love  TANZANIA ni miongoni mwa nchi tatu ambazo zimebahatika kutembelewa...

Makala & Uchambuzi

ZITTO: Hii ndio sababu Malaysia kuushinda umasikini kupitia kilimo, Tanzania ikikwama

Spread the love  MNAMO Februari 2017, miaka sita sasa imepita, niliandika, kupitia...

Makala & Uchambuzi

Ruth Zaipuna: Sekta ya kibenki imeimarika maradufu miaka miwili ya Dk. Samia

Spread the loveTarehe 19 ya mwezi Machi, ni siku muhimu sana kwa...

error: Content is protected !!