December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kidato cha nne waanza mitihani, Rais Samia awatakia kheri

Wanafunzi wa kidato cha nne wakifanya mtihani

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Hassan amewatakia kheri wanafunzi wa kidato cha nne, walioanza mitihani yao ya Taifa leo Jumatatu tarehe 15 Novemba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wanafunzo hao 539,243 wa kidato cha nne nchi nzima, wameanza mitihani yao ya kumaliza masomo baada ya kusotea kwa miaka minne na wataimaliza tarehe 2 Desemba 2021.

Katika ukurasa wake wa Twitter akisema “nawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa kidato cha nne wanaoanza mitihani yao leo.”

“Tunaendelea kujenga nafasi zaidi kwao kusonga mbele kielimu, kiujuzi na kiajira, kwa kuongeza nafasi za kidato cha tano na sita, vyuo vya ufundi stadi na mazingira bora ya nafasi zaidi za ajira.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde

Jana Jumapili, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Dk Charles Msonde alisema vituo 6,090 vya Tanzania Bara na Visiwani vitatumika ambapo kutakuwa na wahitimu 539,243.

Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa 539,243 wa shule ni 502,316 (wavulana 237,776 na wasichana 264,540).

Katibu huyo alisema watahiniwa wa kujitegemea ni 36,927 (wavulana 15,846 na wasichana 21,081).

Idadi hii ya wanafunzi wanaohitimu mwaka huu ni kubwa kuliko ya mwaka jana, ambapo wahitimu walikuwa zaidi ya 400,000.

error: Content is protected !!