January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kidato cha nne kuanza mtihani Jumatatu

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo, Jenista Mhagama

Spread the love

NAIBU Waziri wa Elimu na Ufundi, Jenista Mhagama amewataka maofisa watakaosimamia mitihani ya kidatu cha nne mwaka huu, kutoruhusu kuwapo kwa udanganyifu, imefahamika.

“…natoa wito kwa maafisa elimu wote wa mikoa na halmashauri, kuzingatia sheria za mitihani na kusimamia kwa uangalifu pasipo kuruhusu mianya yoyote itakayoweza kuleta udanganyifu,” alisema Mhagama.

Alisema, tayari nyaraka zote muhimu zitakazotumika katika ufanyaji wa mitihani hiyo, zimeshasambazwa katika wilaya na vituo vyote vyenye watahiniwa nchini.

Kwa mujibu wa Mhagama, mtihani wa kidatu cha nne umepangwa kufanyika, 3 Novemba. Jumla ya watahiniwa 297,488 wameandikishwa kufanya mtihani huo.

Anasema wanafunzi 245,030 ni wanafunzi wa shule na 52,458 ni watahiniwa wa kujitegemea. Watahaniwa 14,723, wamejiandikisha kufanya mtihani wa maarifa.

Amesema, katika kundi la wanafunzi waliopo shule (245,030), wavulani ni 132,244 sawa na asilimia 53.97 na  wasichana 112,786, ambao ni sawa na asilimia 46.03.

Mhagama alisema watahiniwa wa shule watafanya mitihani katika vituo vya shule 4,419 na wale wakujitegemea watafanya mitihani yao katika vituo 920. Watahiniwa wa maarifa wameandikishwa katika vituo 620.

Aidha Mhagama alitoa wito kwa wazazi na jamii yote kwa ujumla kuwa walezi bora kwa watoto wao kwa kuwahimiza katika elimu kwa sababu watoto ndiyo taifa la kesho.

Habari hii imeandikwa na Sarafina Lidwino

error: Content is protected !!