HATIMAYE kichwa kipya cha treni ya umeme chenye namba ya usajili E6800-01 kilichoundwa na kampuni ya ‘Hyundai Rotem Company (HRC) kimewasili nchini Tanzania kutoka nchini Korea Kusini.
Hatua hiyo imekuja baada ya Shirika la Reli Tanzania – TRC kuagiza vichwa vipya 17 vya umeme kutoka ‘Hyundai Rotem Company’ (HRc) ya nchini Korea Kusini vyenye namba ya usajili E6800-01 hadi E6800-17 kwa ajili ya reli ya kiwango cha kimataifa – SGR.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk katika taarifa aliyoitoa kwa umma amesema mfumo wa uendeshaji unaotumika katika kichwa ni nishati ya umeme wenye msongo wa kilovoti 25 na kitakuwa na nguvu ya kilowati 5,000 sawa na nguvu ya 6,800 kwa
kipimo cha “Horse Power.
Amesema kichwa kitakuwa na uwezo wa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa (160km/h), kuvuta na kulisha umeme kwenye mabehewa yasiyozidi 14 ya abiria kwa wakati mmoja.
“TRC Inatarajía kufanya majaribio ya kichwa cha treni kitakachotumika katika rell ya kiwango cha kimataifa kati ya Dar es Salaam na Morogoro na baadaye Dar es Salaam hadi Dodoma, baada ya kukamilisha ukaguzi wa kichwa na mafunzo ya uendeshaji kwa madereva mapema mwezi Disemba 2023.
“Mwezi Disemba 2023 TRC İnatarajia kupokea vichwa vingine vitatu (3), mpango wa uletajl
vitendea kazi utakuwa ukitekelezwa kwa awamu pindi uundwaji wa vitendea kazi
unapokamilika. TRC imeshapokea mabehewa 35 kwa ajili ya uendeshaji wa huduma katika relil ya klwango cha kimataifa.
“Kufikia Septemba 2023 mradi wa SGR Dar es Salaam -Morogoro umefikia 98.6%, Morogoro – Makutupora umefikia 95.41%, Makutupora -Tabora umefikia 12.32%, Tabora-Isaka umefikia 5.02% na Mwanza- Isaka umefikia 41.95%, Mkandarasi kampuni ya CCECC yuko eneo la mradi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza utekelezaji wa mradi wa SGR awamu ya pili Tabora -Kigoma,” amesema.
Leave a comment