Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Kibwana Shomari aongezwa Stars achukua nafasi ya Kapombe
Michezo

Kibwana Shomari aongezwa Stars achukua nafasi ya Kapombe

Spread the love

 

BEKI wa kulia wa klabu ya Yanga, Kibwana Shomari ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe ambaye ameripoti kambini akiwa na majeruhi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikosi hiko kilingia kambini siku ya jana kwa ajili ya kujianda na mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia nchini Qatar 2022, dhidi ya Benin utakaopigwa Oktoba 7, 2021 majira ya saa 1o jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha taarifa hiyo Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Clifford Ndimbo amesema kuwa wachezaji waliongezwa kambini ni Kibwana Shomary na Kibu Denis, mara baada ya Erasto Nyoni, Bakari Mwamnyeto na Shoamri Kapombe kuwapa majeruhi wakiwa na klabu zao.

“Waliongezeka kikosini ambao wameitwa na kocha Mkuu wa kikosi hiko Kim Poulsen ni Kibwana Shomary na Kibu Denis kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majeruhi,” alisema Ndimbo.

Taifa Stars inaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa vinara kwenye kundi J, wakiwa na pointi nne mara baada ya kucheza michezo miwili.

Kibu Denis

 

Akitokea ufafanuzi kuongezwa kwa Kibu Denis ndani ya kikosi hiko Ndimbo, alisema kuwa, mchezaji huyo alikuwepo kwenye mipango ya kocha wa kikosi hiko wakati wa swala lake la uraia likishughulikiwa na uhamiaji.

“Mwalimu alisema kibu yupo kwenye mipango yake ila ishu ya uraia ndio ilkuwa inakwamisha lakini mara baada ya kutatuliwa akawa sehemu ya kikosi na wala hajachukua nafasi ya mtu.” Aliongeza Msemaji huyo.

Mchezaji huyo sakata lake lilihitimika mara baada ya kupewa Uraia Oktoba 2, 2021 na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene kwa mamlaka aliyopewa kwa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002).

Hii itakuwa mara ya pili kwa Kibu Denis kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, mara baada ya kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Malawi uliopigwa Juni 13, 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!