MAZISHI ya aliyekiwa mtangazaji wa Kituo cha Redio Clouds, Ephrahim Kibonde atazikwa Jumamosi wiki hii. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).
Mwili wa Kibonde unatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7, saa nne usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuzikwa Jumamosi.
Joseph Kusaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group ametoa taarifa hiyo leo tarehe 7 Machi 2019 na kwamba, mwili wa Kibonde unatarajiwa kutua Dar es Salaam saa 4 usiku wa leo.
Amesema, baada ya kufika mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.
“Jana usiku niliongea na daktari Derrick aliyekuwa anamtibu Ephraim Kibonde akanihakikishia kuwa anaendelea vizuri lakini bahati mbaya wakati tunajiandaa kurudi Dar es Salaam hali ikabadilika na kusabaisha kifo chake.
“Taratibu za mazishi na maombolezo, zinafanyika nyumbani kwake Mbezi na tunatarajia kuaga na kumpumzisha siku ya Jumamosi katika makaburi ya Kinondoni karibu na kaburi la mke wake,” amesema Kussaga.
Leave a comment