August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kibatala: Mbowe hajashindwa kesi

Freeman Mbowe (kulia) na Jenerali Ulimwengu (katikati) na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob

Spread the love

PETER Kibatala Wakili Mwandamizi wa Chama Cha Demokrasia (Chadema), ameweka wazi kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema la kumfungulia kesi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wengine watatu, anaandika Faki Sosi.

Walalamikiwa wengine kwenye kesi hiyo namba moja ya mwaka 2017 ni Simon Sirro, Kamshina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Mkuu wa Upepelezi, Cammillius Wambura na George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kibatala aliueleza mtandao huu, kuwa mahakama chini ya jopo majaji watatu wakiongozwa na Sekieti Kihiyo, akisaidiana na Jaji Lugano Mwandambo pamoja na Jaji Pellagia Kaday, imekubali ombi la Mbowe kufungua shauri hilo kwenye mahakama hiyo na kutoa zuio la kutokamatwa kwa mwenyekiti huyo hadi usikilizwaji wa kesi ya msingi ya kikatiba utakapokamiliaka.

Kibatala amesema Mahakama imetolea uamuzi juu ya maombi hayo madogo kuwa yanaondolewa mahakamani hapo kutokana na kifungu kilichotumika kuwa sio sahihi. “Hivyo basi kuondolewa huko kwa maombi hayo haifungi milango ya kuleta tena maombi hayo kwa Sheria nyingine ambayo uamuzi huo haijautaja.”

Hata Mawakili upande wa utetezi ambao walikuwepo mahakamani ,uliongozwa na Kibatala pamoja Jenerali Ulimwengu walitolea ufafanuzi kuwa maombi hayo yalipelekwa kwa kifungu 2(3) cha Sheria ya (Jala) inayosema Mahakama gani inamlaka juu ya jambo husika na kwamba maombi hayo kwa jinsi yalivyo ni kipengele hiko kinaweza kutumika. Hata hivyo mawakili hao wanasema watayarudisha maombi hayo kesho mapema.

Mbowe amefungua kesi ya kupinga ukeukwaji wa katiba na Sheria juu ya kitendo cha Makonda kuwataja watu majina hadharani washukiwa wa madawa ya kulevya kinyume matakwa ya taratibu za sheria na katiba. Kesi hiyo itaendelea Machi 8, 2017.

error: Content is protected !!