Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kibatala apinga ushahidi wa kamera Mahakamani kesi ya Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Kibatala apinga ushahidi wa kamera Mahakamani kesi ya Mbowe

Spread the love

WAKILI upande wa utetezi Peter Kibatala amepinga kupokelewa kwa kielelezo cha kamera na tape mbili za kurekodia video (Min-Dv) zilizotolewa kwenye ushahidi kwa upande wa Jamhuri mahakamani Kisutu  katika kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018, ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa  chama hiko akiwemo Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema)-Taifa, Vicent Mashinji Katibu Mkuu Chadema)-Taifa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Bara  Salumu Mwalim Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini , Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini, Halima Mdee , Mbunge wa Kawe, Mbunge , John Heche Mbunge wa Tarime Vijijini, na Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini.

Shahidi huyo wa sita aliyejitambulisha mahakamani hapo kwa jina la F5392 Koplo Charles  ambaye askari anayefanya kazi kwenye Ofisi ya Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, mwenye jukumu la kuhifadhi na kuchukua matukio mbalimbali kwa njia ya kamera kama ushahidi na vielelezo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba , wakili wa serikali mkuu Paul Kadushi amemuongoza shahidi huyo kutoa ushahidi wake.

Licha ya kadushi kumuongoza shahidi pia ameongoza mawakili wa  wakuuu wa Serikali pamoja na Faraja Nchimbi, Dk. Zainabu Mango, Wankyo Simon, na Jackline Nyantori.

Upande Utetezi uliongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, Hekima Mwasipu,  na John Mallya.

Awali shahidi huyo alieleza mahakama kuwa siku ya tarehe 16 Februali akiwa kwenye Ofisi za Mkuu wa Upelelezi alipangiwa jukumu la kukusanya matukio kwa njia ya kamera kwenye kampeni za uchaguzi mdogo kwenye jimbo la Kinondoni .

Ameeleza kuwa alipangiwa kukusanya matukio ya video kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni za Chadema zilizofanyika katika viwanja vya Buibui eneo la Mwananyamala.

Ameeleza kuwa alihakiki kamera yake aina ya Sony  DV-CAM kuwa ipo sawa kwenye upande wa picha, sauti, na kuwa chaji ya kutosha kwenye betri itakayo muwezesha kuitumia kwa  saa 4 hadi 9.

Shahidi amedai kuwa alifika kwenye mkutano huo saa 10 jioni na kuanza kurekodi baada ya mkutano huo kuanza mabapo alisikia wabunge na viongozi wa Chadema wakitoa maneno yaliyowahamasiha na kuwa jazba wananchi walikuwa pale juu ya kuichukia serikali na vyombo vya usalama.

“Baada ya kukabidhiwa Mwenyekiti jazba ilizidi waliokuwa wamekaa wamesimama jazba iliongozeka kwa asilimia zaidi na mwisho akasema tutaondoka tutakwenda kwa mkurugenzi” amedai shahidi huyo.

Shahidi huyo amedai kuwa viongozi hao waliamrisha wafuasi wao waelekee kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, yeye aliposhindwa kuendelea kurekodi kwa sababu ya vurugu za mawe na miti yaliyorushwa na wafuasi wa chama hicho akalazimika kurudi Ofisini kwake na kuripoti kwa Mkuu wa upelelezi aliyekuwa kashaapata habari  kuhusu kampeni hizo.

Baada ya  hapo shahidi huyo huku akiongozwa  na wakili Kadushi  alihojiwa kuhusu hali ya kamera na vifaa alivyovitumia kurekodia alivyoviita Dv tape (tape za kurekodia).

Baada ya hapo Wakili Kadushi aliomba kuwasilisha vielelezo hivyo mabyo ni kamera na tape mbili zilizodaiwa kurekodia tuko la ufunguzi wa kampeni za Chadema.

Upande wa utetezi umepinga kupokelewa kwa kielelezo cha Jamhuri juu ushahidi wa kamera na tape mbili za kurekodia video Min-Div .
Upande huo ulitaka Jamhuri iwasilishe kiapo maalum kwa ajili ya kutoa vielelezo hivyo kama yalivyo matakwa ya sheria fungu la 18 na 19 la sheria ya ushahidi wa kieletroniki.

Upande  wa utetezo ulitaka Jamhuri iwasilishe kiapo maalum kwa ajili ya kutoa vielelezo hivyo kama yalivyo matakwa ya sheria fungu la 18 na 19 la sheria ya ushahidi wa kieletroniki.

Wakili Peter Kibatala amepinga kupokelewa kwa vielelezo hivyo mahakamani hapo akidai kuwa ni lazima kuwepo kwa uthibitisho na kiapo mahusiisi juu ya vielelezo hivyo.

Tunapinga Ushahidi wa kieletronik hata maelezo ya shahidi amesema ni digital kamera ambapo ni wazi kuwa ni eletronic.

Akirejea kwenye uamuzi wa mahakama ya rufaa katika kesi ya Nangole ulioikata ushahidi wa eletroniki na kuvitaka vitu kama Flash, na simu ni divive zinazoingiankwenye mifumo ya Komputer vinavyotoa chukua n kupokea.
Majaji walitoa walikataa ushahidi huo unatoka na mifumo ya kikompyuta mashart ya 18 na 19 cha ushahidi wa kieletroniki.

Kesi ya madai namba 6 ya 2015 ya Emmauel Mwasonga kwamba kabla ya shahidi kula kiapo alitakiwa awe na kiapo mahususi kwa ajili ya kutoa ushahidi wa kieletroniki.

Paul Kadushi wakili wa Serikali aliiomba mahakama kuiahilisha kesi hiyo ili kesho yake ambapo kesi hiyo itaendelea watarejea na hoja juu ya pingamizi na utetezi .

 Hakimu Simba meahilisha shauri hilo mpaka kesho saa 4:00 asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!