March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kibatala amnasua Sugu

Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga katika kesi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa kosa kutumia lugha ya fedheha kwa Rais John Magufuli ambapo walinyimwa dhamana kutokana upande wa jamhuri kupinga dhamana yao mahakamani hapo.

Leo wakili wa utetezi Peter Kibatala aliieleza mahakama kuwa upande wa Jamhuri hauna hoja za kuendelea kushikilia dhamana ya watuhumia kutokana na kufunga pazia la ushahidi mahakamani.

Upande wa Jamhuri umewasilisha mashahidi sita mahakamani hapo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Michael Mteite, amewapa dhamana watuhumiwa hao.

Watuhumiwa hao walijidhamini wenyewe kwa kusaini hati ya Sh. Milioni tano kila mmoja.

Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kuwasilisha majumuisho ya shauri hilo tarehe 19 Februari.

Kesi hiyo itatajwa tena Februari 26 mwaka huu ambapo mahakama hiyo itatoa hukumu ya kwamba Sugu na mwenzie wana hatia au laa.

Kama mahakama itawakuta na hatia watuhumiwa hao wanalazima kujitetea kama haikujiridhisha kuhusu tuhuma hizo itawaachia huru.

error: Content is protected !!