July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kibano watumishi hewa chaanza

Spread the love
JORDAN Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewaagiza wakurugenzi na wakuu wa idara katika mkoa huo kutoa maelezo ya kina sababu za kuruhusu kuwepo kwa watumishi hewa 144, anaandika Dany Tibason.
Rugimbana ametoa agizo hilo leo wakati wa makabidhiano ya ofisi kati yake na Chiku Ghalawa, aliyekuwa mkuu wa mkoa huo ambaye amehamishiwa Mkoa wa Songwe.
Akizungumza na wakuu wa idara, viongozi wa dini, wazee maarufu na viongozi wa vyama vya siasa Rugimbana amesema, ni aibu kwa Mkoa wa Dodoma kuwa na watumishi hewa.
Akizungumzia mikakati yake amesema, amepelekwa Dodoma kwa ajili ya kufanya kazi ya wananchi na kutatua kero za sambamba na kuhakikisha wanapata maendeleo.
Amesema, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano hataweza kumwonea haya mtumishi yoyote ambaye ataonekana kukwamisha shughuli na mikakati ya maendeleo katika Mkoa wa Dodoma.
Galawa amemweleza Rugimbana kuwa Mkoa wa Dodoma ni wa kwanda kuwa wa watu waliodumaa kiakili.
Amesema, kudumaa kiakili kunatokana na wakazi wa mkoa huo kukosa lishe bora kwa mama wajawazito.
“Hata tukiboresha miundombinu ya aina gani ya kielimu lakini kama hakuna lishe bora na yenye virutubisho kwa akina mama wajawazito, ni wazi hapatakuwepo na maendeleo yoyote.
“Mkoa wa Dodoma unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuwa na watu waliodumaa kiakili, ombaomba pamoja na kutokuwa na miundombinu bora ya kielimu.”
error: Content is protected !!