Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kibano; Wakili Chadema Vs Shahidi Jamhuri
Habari za SiasaTangulizi

Kibano; Wakili Chadema Vs Shahidi Jamhuri

Spread the love

SHAHIDI  wa kwanza kwenye ya kesi uchochezi  inayowakabili viongozi wa Chadema, ameeleza kwamba hajui sababu za muuaji wa Akwelina Akwilini kutofikishwa mahakamani mpaka sasa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Shahid huyo ametambulishwa kuwa ni SSP Gerald Ngichi, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kinondoni. 

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu tarehe 17 Aprili, SSP Ngichi ameeleza kuwa, hajui kwanini hadi leo hakuna mtuhumiwa yeyote aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya Akwili, aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Tarehr 16 Februari mwaka 2018, siku ambayo viongozi wa   Chadema na wafuasi wao walifanya maandamano kupinga mawakala wao kutoapishwa kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni. Maandamano hayo yalinadaiw kupelekea kifo cha Akwelina.

Yafuatayo na mahojiano kati ya Wakili wa utetezi Peter Kibatala na shahidi wa Jamhuri SSP Ngichi.

Wakili Kibatala: Shahidi nimekusikia kwamba, umeanza kutumikia jeshi la Polisi tangu 2000.

Shahidi: Sawa

Wakili Kibatala: Una elimu gani?

Shahidi: Shahada ya Udhamili ya Utawala kutoka Chuo cha Mzumbe.

Wakili Kibatala: Shahada yako ilikuwa ya nini?

Shahidi: Ya Sheria daraja la pili, niliipata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wakili Kibatala: Naongea na mtu mwenye ufahamu wa sheria?

Shahidi: Ndio.

Wakili Kibatala: Ulizungumzia kifo cha Akwilina, majina yake tafadhali?.

Shahidi: Siyajui.

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba ofisa ambaye uliongoza operesheni, mwenye kujua sheria humjui mtu uliyemtaja kwenye maelezo yako alijeruhiwa kwenye maandamano?.

Shahidi: Namjua Akwelina .

Wakili Kibatala: Nataka majina mawili. Una uhakika gani kwamba unayemtolea ushahidi ndiye huyu huyo uliyemtaja kwa sababu kuna Peter na Peter Kibataka.

Shahidi: Nitamuomba muongoza mashataka.

Wakili Kibatala: Shahidi ulimuona mwendesha mashtaka ndio shahidi, wewe ndio uliyekula kiapo.

Wewe ndio ulikuwa mkuu wa Operesheni, unaweza kuieleza mahakama chanzo cha kifo cha Akwelina?

Shahidi: Siwezi kujua. Sababu ya kifo cha Akwilin anapaswa kujua ni mpelelezi

wa kifo.

Wakili Kibatala: Ukiwa kama ni ofisa wa operesheni na ulikuwa ndio unaongoza vikosi, ni nini sababu ya kitabibu ya kifo cha Akwilina?

Shahidi: Mimi siijui.

Wakili Kibatala: Sasa kama hujui sababu ya kifo, nini kilichokufanya useme marehemu amekufa kutokana na tukio la maandamano?

Wakili Kibatala: Unafahamu dhana ya ‘hear say’ ni sawa na umbea.

Shahidi: Hapana.

Wakili Kibatala: Mimi nasema ni umbea, wewe hujakiona, hujakishuhudia.

Shahidi: Mimi nasema sio umbea maneno ya kuambiwa.

Wakili Kibatala: Ni sahihi yale  yote uliyoyasema juu ya Akwilina wewe huyajui, kuna watu wengine waje waseme.

Shahidi: Sawa.

Wakili Kibatala: Hitimisho la kwamba, Akwelina alikufa kwenye maandamano?

Shahidi: Sio sahihi. Sio kila ninalosema mahakamani nimeshuhudia, mengine yameripotiwa kituoni.

Wakili Kibatala: Unajua sababu ya kifo cha Akwilina, alikufa kwa mshutuko au alipomuona Mbowe?

Shahidi: Sijui.

Wakili Kibatala: Unakubaliana na mimi kuwa wewe hujui chochote kuhusu kifo cha Akwilin, unataka aje mtu mwengine kutoa taarifa hizo?

Shahidi: Sawa.

Wakili Kibatala: Unaufahamu binafsi kuhusu taarifa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam juu ya kifo cha Akwelina?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Kibatala: Mtu akifariki katika kifo kisichojulikana sababu zake lazima upite uchunguzi, watu waliohusishwa kupelekwa mahakamani. Ni nani aliyeshitakiwa kwa kosa la mauaji ya Akwelina?

Shahidi: Hakuna .

Wakili Kibatala: Ni hali ya kawaida  mtu anakufa katika mazingira ya kutatanisha na hakuna mtu yoyote alipelekwa mahakamani?

Shahidi: Kimya

Wakili Kibatala: Ulishawahi kuona mtu amefariki katika mazingira ya kutatanisha na hakuna aliyepekwa mahakamani kwa kesi ya mauaji ya kukusudia au mauaji ya bila kukusuadia.

Shahidi: Wapi nje au ndani ya nchi?

Wakili Kibatala: Kesi hii imetokea ndani ya Tanzania?.

Shahidi: Kama kuna mtu amefanya kitendo kama hicho tunachukua hatua.Tukio kama hilo linapelelezwa na hatua nyengine zinafuatiwa.

Wakili Kibatala: Umejibu swali lingine. Nakuuliza, umewahi kushuhudia kifo kama cha Akwelina na hakuna mtu anayepelekwa mahakamani.

Shahidi: Sijawahi kushuhudia huyo Akwelina anauawa.

Wakili Kibatala: Nakuuliza kwa mara ya saba kwa uzoefu wako wa miaka 20, ushawahi kushuhudia mtu anauawa eneo la wazi kama Kawawa (barabara ya Kawawa) na hakuna mtu yeyote aliyepelekwa mahkamani?

Shahidi: Sijawahi kushuhudia.

Hakimu Simba ameuambia upande wa mashtaka muongozeni shahidi ajibu swali.

Wakili Nchimbi (Upande wa Mshtka):Jibu moja kwa moja (straight)

Shahidi: Sijawahi kushuhudia mtu anakufa eneo la Kawawa.

Wakili Kibatala: Ulizungumzia watu walikuwa wameogofywa (wameogopa) wengine wakafunga maduka na wengine walikimbia, hawa watu uliwahi kuongea nao binafsi?.

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Uliongea nao wapi,kituoni Osterbey au eneo la tukio?.

Shahidi: Eneo la tukio.

Wakili Kibatala: Baada au kabla ya maandamano?

Shahidi: Baada ya maandamano nilibaki nikaongea nao.

Wakili Kibatala: Ni wapi?.

Shahidi: Kushoto na kulia mwa barabara ya Kawawa.

Wakili Kibatala: Eneo gani?

Shahidi: Mkwajuni.

Wakili Kibatala: Ni sahihi Ofisa wa Polisi hajiongozi wenyewe kuna kitabu maalumu kinachowaongoza kinaitwa (GPO).

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Wewe unatakiwa uwe na Notebook kwa mujibu wa GPO.

Shahidi: Ndio.

Wakili Kibatala: Bila shaka uliona umuhimu wa kuchukua maelezo ya wafanyabiashara wa barabara ya Kawawa uliowahoji .

Shahidi: Hapana.Sio kila unayemuhoji unaandika.

Wakili Kibatala: Shitaka  namba nne Umma Kupata uwoga ndio maana nakuuliza maswali.

Sasa tukubaliane na maelezo ya hawa watu waliogofywa ambao uliwahoji wewe uliyarekodi?.

Shahidi: Sikurekodi.

Wakili Kibatala: Wakati unaongozwa na wakili wa serikali ulisema watoto na wazee walipotea, unaufahamu binafsi juu hao wazee.

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Uliwahoji wewe?

Shahidi: Askari mbalimbali kwenye vituo mbalimbali vya polisi.

Wakili Kibatala: Vituo gani vitaje

Shahidi: Hananasifu na Mwananyamala.

Wakili Kibatala: kutoka eneo la tukio kuna umbali gani mpaka kituo cha Polisi?

Shahidi: Kama mita 900.

Wakili Kibatala: Mwambie hakimu kama unakumbuka majina ya Polisi waliorekodi maelezo ya watoto na wazee hawa.

Shahidi: Askari wa zamu waliokuwepo vituoni.

Wakili Kibatala: Unayajua majina yao?

Shahidi: Siyafahamu .

Wakili Kibatala: Umesema katika maelezo yao kuwa, maduka na stoo zilivamiwa na kuibiwa. Chagua majina matano tu uyataje yaliyoporwa?

Shahidi: Majina ya maduka yaliyofanyiwa uhalifu yapo kwa mpelelezi.

Wakili Kibatala: Hayo maduka na hizo stoo unayafahamu majina yake au huyafahamu?

Shahidi: Kumbukumbuka za Jeshi la Polisi zipo .

Wakili Kibatala: Unayafahamu au huyafahamu?

Shahidi: Sizikumbuki.

Wakili Kibatala: Maandamano uliyazuia kwa sababu kuwa ofisi za mkuregenzi, ulifahamu kuwa  saa moja ofisi zilikuwa wazi?

Shahidi: Ninafahamu kuwa zilifungwa.

Wakili Kibatala: Unaufahamu wowote juu ya ofisi ya mkuregenzi wa Manspaa muda wa saa 11 zilikuwa wazi ambapo wewe ulidai kuwa, muda huo umesimisha maandamano?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Kibatala: Unafahamu majina ya Mkurugenzi wa Manspaa?

Shahidi: Nalifahamu lakini nimesahau.

Wakili Kibatala: Hapo awali ulisema kuwa, ulipewa taarifa na wasimamizi wa uchaguzi unajua majina ya maofisa hao?

Shahidi: Siwafahamu.

Wakili Kibatala: Ulichukuwa maelezo ya Mkurugenzi wa Manspaa kuhusiana na tukio hilo?.

Shahidi: Hapana sikuchukua.

Wakili Kibatala: Unaufahamu juu ya ofisa wako yeyote aliyechukuwa maelezo ya Mkurugenzi wa Manispaa  juu ya tukio hilo kuhusiana na ofisi kufungwa.

Shahidi: Hapana.

Wakili Kibatala: Ulichukua maelezo ya Msimamizi wa Uchaguzi kuhusiana na kufungwa ofisi?

Shahidi: Sikuchukua.

Wakili Kibatala: hakuna ofisa yoyote  uliyekuwa naye aliyechukuwa maelezo ya Msimamizi wa Uchaguzi?

Shahidi: Hawakuchukua.

Wakili Kibatala: Ulisema kampeni pekee ndio zilizoruhusiwa ni kipi kilichokujuza wewe kuwa watu wa Chadema wameruhusiwa kufanya kampeni pekee yake.

Shahidi: Barua.

Wakili Kibatala: Umeitoa kama kielelezo mahakamani?

Shahidi: Hapana.

Wakili Kibatala: Sasa hatuna barua hatuna ratiba, tunawezaje kuthibitisha kuwa kulikuwa na kampeni siku hiyo bila barua bila ratiba?

Shahidi: Kimya.

Wakili Kibatala: Kwa kuwa hatuna hizo nyenzo hizo mbili mahakama itawezaje kujua Chadema waliruhusiwa kufanya hiki na hiki?.

Shahidi: Barua kwa sasa haipo lakini mahakama ikitaka nitaileta.

Wakili Kibatala: Kwani wewe ni mwendesha mashataka?

Shahidi: Hapana.

Wakili Kibatala: Shitaka la nne linasema, watuhumiwa ni viongozi tisa wa Chadema na watu wengine 12  ambao hawapo mahakamani walifanya kusanyiko lisilo halali, wewe umesema ni kati ya watu 600 na 700. Kati ya wewe na hati ya mashtaka nani muongo?.

Shahidi: Mimi ninachosema ndio kilichopo.

Wakili Kibatala: Ulisema PC Fikiri na Koplo Msangi walipata majeraha ya aina gani?

Shahidi: Mmoja alijeruhiwa kichwani mmoja mguuni mwengine mgongoni.

Wakili Kibatala: Ukiwa kama ofisa mzoefu wa miaka 20 ndani ya jeshi bila shaka walipopata majeraha waliandikwa taarifa gani?

Shahidi: Waliandikiswa taarifa ya kupota majeraha na kesi iliyofunguliwa ni kujeruhi kwa madhara makubwa.

Katika kitabu PGO ni lazima tukio lolote la kijinai liingie kwenye RB tukio hilo liliingizwa .

Wakili Kibatala: Nani alirekodi?

Shahidi: Askari wa zamu.

Wakili Kibatala: Unamfahamu askari aliyerekodi maelezo ya askari  hao waliojeruhiwa?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Kibatala: Unafahamu kuwa Msangi aliwekwa ndani (mahabusu)kwa muda juu ya kifo cha Akwelina?

Shahidi: Sijui.

Wakili Kibatala: Kama unafahamu kama alipelekwa rumande ni lini alipelekwa?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba kuna askari walikamatwa na kuwekwa ndani siku kadhaa kuhusiana na kifo cha Akwilina?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Kibatala: Hujui kama kuna askari  walikamatwa?

Shahidi: Sifahamu.

Wakili Kibatala: Fikiri na Msangi walikuwa moja ya askari waliofyatua risasi.

Shahidi: Hawa walijeruhiwa kabla  na kuondolewa eneo la tukio.

Wakili Kibatala: Tutajie majina ya maofisa wa polisi waliofyetua risasi kwa amri yako.

Shahidi: Ninawafahamu lakini sina kumbukumbu ya majina yao hapa mahakamani.

Wakili Kibatala: Unajua idadi risasi?

Shahidi: Ninajua idadi ya risasi zilizofyetuliwa lakini sina idadi ya risasi hapa (kwa sauti ya juu).

Wakili Kibatala: Unafahamu mahali ambapo risasi zote zilizopokwenda.

Shahidi: Baadhi sifahamu baadhi nafahamu.

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwa mujibu wa GPO (kitabu cha muongozo cha Polisi) askari wanalazimika kurejesha silaha kwa rekodi na kuondoka nazo kwa rekodi kwa kujua askari fulani alichukua silaha namba fulani?.

Shahidi: Sahihi.

Wakili Kibatala: Kuna risasi ulizihesabu? sheria inasema kuwa lazima uhesabu risasi ni sahihi kuwa kuna risasi zilipotea na nyengine zilipatika. Mlitoleaje maelezo ya risasi zilizopotea.

Shahidi: Tunaandika tumempa askari risasi 30 kama zimerejee 15, tunandika 15 kwa 30.

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba kuna watu watano walijeruhiwa na Jeshi la Polisi na kwamba, walikaa polisi mahabusu ya Osterbey siku 14?.

Shahidi: Sina taarifa.

Wakili Kibatala: Ni sahihi pamoja na mambo mengine kuna kuwa na kitambaa ndani ya ILANI ambacho kina maneno ambayo ni maalumu ambayo ni muhimu?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Kibatala: Ni sahahi wewe ndio mwenye mamlaka na kitaambaa cha ILANI?

Shahidi: Ndio.

Wakili Kibatala: Tumekubaliana ni kitambaa cha kisheria na ni muhimu na ile amri ya polisi iwe halali na umwambie hakimu kuwa, uliongozwa na wakili wa zerikali kutamka maneno yaliyokuwepo kwenye kitambaa cha ILANI?

Shahidi: Kile kitambaa ni maelekezo ya kipolisi .

Wakili Kibatala: Umeongozwa au hujaongozwa?

Shahidi: Sijaongozwa.

Wakili Kibatala: Dereva wako ulimtaja?

Shahidi: Sijamtaja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!