January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kibamba: UKAWA wanaimudu CCM

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akiwa anatafakari bungeni

Spread the love

MTAFITI na mchambuzi wa masuala ya demokrasia Kanda ya Afrika Mashariki, Deus Kibamba amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ndivyo vinafaa zaidi kupambana katika ngazi ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mpaka sasa vyama vya upinzani ambavyo havijafungamana na Ukawa vilivyochukua fomu ya kuwania urais ni; Democratic Party (DP) kikiwakilishwa na Mchungaji Chrisopher Mtikila, UPDP kikiwakilishwa na Fahmi Dovutwa, TLP kikiwakilishwa na Maxmilian Lyimo na ADC kikiwakilishwa na Hamad Rashid huku ACT – Wazalendo kikiwa kimya.

Kibamba amesema “Mimi nadhani wangeacha ligi ya urais iwe kati ya CCM na Ukawa. Hawa ndio wana nguvu zaidi katika siasa kwa sasa. Mfano leo Mwenyekiti wa TLP, Agustino Lyatonga Mrema hata akigombea udiwani hawezi kushinda. Hiyo ni dalili kwamba amekwisha kisiasa.”

“Kugombea urais haimanishi ndio demokrasia. Uwezo wao katika siasa bado ni mdogo. Watanzania kwa sasa wanahitaji mabadiliko. Kwa vyama hivyo vidogovidogo kugombea urais ni sawa na kumega kura za Ukawa na kuchelewesha mabadiliko,” amesema Kibamba.

Aidha, Kibamba ameshauri kwamba kwa sasa vyama hivyo ambavyo vingejikita zaidi kujiimarisha kwa kugombea nafasi ya ubu nge na udiwami.

error: Content is protected !!