Monday , 22 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kiama cha madalali na wenye nyumba chaja
Habari Mchanganyiko

Kiama cha madalali na wenye nyumba chaja

William Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Spread the love

KIAMA cha madalali wa kupangisha nyumba na wamiliki wa nyumba za kupangisha kinakuja baada ya serikali kukusudia kupeleka mswada wa sheria bungeni wa kuwataka nao kulipa kodi, anaandika Nasra Abdallah.

Sambamba na hilo pia wamiliki wa nyumba watatakiwa kuwalipisha wateja wao kodi za mwezi mmoja mmoja kama wanavyofanya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) badala ya mwaka au miezi sita.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipokuwa akifungua rasmi jengo la ofisi za makao makuu ya shirika hilo lililopewa jina la ‘Kambarage House’, hafla iliyoendana sambamba uwekaji wa mnara wenye sanamu ya Mwalimu Nyerere.

Lukuvi amesema kitendo cha madalali na wapangishaji kufanya kazi hiyo bila ya serikali kupata kodi wakati wao wanapata fedha nyingi hakikubaliki ukizingatia kwamba serikali ya sasa imeweka nguvu kubwa katika ukusanyaji kodi.

Kama vile haitoshi amesema kuna baadhi ya kampuni na taasisi zinafanya kazi hizo za kupangisha na ni walipaji wazuri wa kodi, hivyo ni vema nao wakaingia katika mfumo huo ili kazi hiyo iweze kutambuliwa rasmi badala ya kila mtu kufanya vile anavyotaka.

Wakati kwa upande wa wenye nyumba amesema baada ya sheria hiyo kupitishwa watalazimika kuwatoza wapangaji wao kodi kila mwezi badala ya miezi sita au mwaka kama wanavyofanya kwa sasa.

”Kwa muda mrefu sasa tumegundua kuna tatizo katika sekta hiyo ya upangishaji nyumba ikiwemo watu wanaoenda kuanza maisha maeneo mapya auvijana wanaoanza maisha kushindwa kupangisha karibu na mjini wanapofanyia kazi kutokana na kodi kuwa kubwa.

“Mbaya zaidi ni kutakiwa kulipa kwa miezi sita au mwaka wakati hata hela ya kula kwake shida na ninaahidi hili nitalisimamia kwa nguvu zangu zote na ole wake atakayebainika kukiuka shria hiyo itakapopitishwa,’alionya Lukuvi.

Akiwageukia NHC, Waziri Lukuvi aliwataka wakati wakiwa wanaendelea kutekeleza miradi ya nyumba za kuuza wasisahau kuacha na nyumba za kupangisha kwa kuwa bado mahitaji yake ni makubwa na kuongeza kwamba kwa kutofanya hivyo kuna siku watajikuta hawana nyumba wanazomiliki.

Kuhusu jengo alilifungua alisema anategemeo kuona ufanisi unaoendana na jingo hilo, kwa kuwa sasa wafanyakazi hawatakuwa na sababu ya kutofanya kazi kwa weledi kwani wana mazingira mazuri ya kufanyia kazi ikiwemo vitendea kazi.

Awali akimkaribisha Waziri huyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema moja ya sababu ya kuweka sanamu la Mwalimu Nyerere nje ya jengo hilo, ni kama moja ya kutambua mchango wa Mwalimu Nyerere katika sekta ya nyumba na na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo kuweza kuijua sura ya mhasisi huyo wa Taifa hili.

Wakati kuhusu jengo alisema ni kutokana na mabadiliko makubwa waliyoamua kuyafanya katika shirika hilo kwa suala zima la uwekezaji ambapo wameweza kushiriki na benki mbalimbali katika utekelezaji wa miradi yao mbalimbali.

“Mojawapo ya jambo litakalokufanya uaminike katika kukopesheka ni pamoja na muonekano wako, hivyo kwetu sisi hili jengo ni kielelezo tosha cha kuwaaminisha watu kwamba tunaweza kukopesheka pasipo na shaka na pia litasaidia wafanyakazi wetu kufanya kazi katika mazingira mazuri,”alisema Mchechu.

Jengo hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 13,810, Mkurugenzi huyo alisema limejengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 29 ikiwa ni pamoja na uwekaji wa samani za ndani za ofisi na ni jengo lililopewa kibali cha majengo yaliyozingatia mazingira (green building), ambalo linatumia umeme na maji kidogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 767.2 za dawa za kulevya, 21 mbaroni

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!