Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo Soka Kessy ajiunga Mtibwa akitokea Nkana FC
Soka

Kessy ajiunga Mtibwa akitokea Nkana FC

Spread the love

TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro nchini Tanzania, imemsajili beki Ramadhan Kessy akitokea Nkana FC ya Zambia. Anaripoti Kelvin Mwapungu, Dar es Salaam…(endelea)

Mtibwa iliyomaliza vibaya msimu wa 2019/20 imemtangaza Kessy leo Jumapili tarehe 30 Agosti 2020 kuwa mchezaji wake.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Mtibwa wameweka picha za Kessy na kuandika “Kessy ndani ya nyumba.”

Kisha wakasema “Leo tumefanikisha kuinasa saini ya beki bora kabisa wa upande wa kulia Hassan Khamis Ramadhan Kessy.”

“Tumemsajili Hassan akitokea mabingwa wa ligi kuu ya Zambia msimu 2019/2020 Nkana Red Devils. Huu ni usajili wetu wa tano msimu huu katika kuboresha kikosi,” imesema Mtibwa

Kessy aliyezaliwa tarehe 25 Desemba 1994 mkoani Morogoro nchini Tanzania alijiunga na Nkana FC msimu wa 2018/19 akitokea Yanga ya Dar es Salaam.

Beki huyo kisiki upande wa kulia, alijiunga na Yanga 2016 akitokea kwa watani zao Simba.

Kessy alijiunga na Simba mwaka 2014 akitokea Mtibwa aliyoitumikia kwa miaka takribani mitatu kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 alipotimkia Simba.

Hii ina maana kwamba, Kessy amerejea katika timu aliyowahi kuichezea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoSokaTangulizi

Simba SC. yang’ara, yawakung’uta 2:0 wahabeshi

Spread the loveKILELE cha Sherehe ya Siku ya Simba ‘Simba Day’ kimetamatika...

MichezoSokaTangulizi

Manara, Hersi kizimbani TTF

Spread the loveSEKRETARIETI ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) imewafungulia...

error: Content is protected !!