Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kesi ya Zuma: Rais Ramaphosa kuhojiwa mahakamani
Kimataifa

Kesi ya Zuma: Rais Ramaphosa kuhojiwa mahakamani

Jacob Zuma
Spread the love

 

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amejumuishwa katika uchunguzi wa tuhuma za ufisadi, zinazomkabili kiongozi wa zamani wa Taifa hilo, Jacob Zuma. Inaripoti BBC … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao huo, leo Jumatano, tarehe 11 Agosti 2021, Ramaphosa ameitwa mbele ya jopo la uchunguzi wa tuhuma hizo, zinazomkabili Zuma ambaye kwa sasa yuko rumande, kwa kosa la kukaidi wito wa mahakama wa kushiriki uchunguzi dhidi yake.

Rais Ramaphosa amejumuishwa katika uchunguzi huo, kwa kuwa alikuwa Naibu Kiongozi wa Chama Tawala cha ANC, wakati Zuma akiwa madarakani.

Hivyo, atahojiwa ili kujibu hatua zilizochukuliwa na chama hicho tawala, wakati Zuma anatenda kosa hilo la kufanya ufisadi.

Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini

Jopo la uchunguzi hilo, linahitaji kujua kutoka kwa Rais Ramaphosa, kama chama hicho kilichukua jitihada zozote kumzuia Zuma asitende kosa hilo, alipokuwa madarakani.

Katika kesi hiyo ya ufisadi inayomkabili Zuma katika Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini, mwanasiasa huyo anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya.

Kufuatia hatua yake ya kuruhusu familia ya kitajiri iliyotajwa kwa jina la Gupta, kupora rasilimali za Serikali.

Kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini, anadaiwa kufanya ufisadi wa Dola za Marekani 81 bilioni. Lakini pia, anadaiwa kutumia mamlaka yake vibaya, kwa kuteua baraza la mawaziri kwa maslahi yake binafsi.
Hata hivyo, Zuma na familia hiyo wamekanusha kuhusika na tuhuma hizo.

Zuma aliingia madarakani 2009 na kuiongoza Afrika Kusini kwa miaka tisa mfululizo, hadi 2018 alipojiuzulu kwa tuhuma za ufisadi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!