Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya wahariri Mawio, Lissu yaahirishwa, kusikilizwa kesho
Habari MchanganyikoTangulizi

Kesi ya wahariri Mawio, Lissu yaahirishwa, kusikilizwa kesho

Wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrissa wakibadilishana mawazo na viongozi wa kampuni ya Flint waliokuwa wachapishaji wa gazeti hilo
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imehairisha usikilizwaji wa awali wa kesi ya uchochozi inayowakabili wahariri wa gazeti la Mawio, mbunge wa Chadema na mchapishaji wa magazeti, anaandika Faki Sosi.

Kuahirishwa kwa kesi hiyo kunatokana na upande wa mashitaka kutokamilisha maelezo ya awali. Imeahirishwa hadi kesho .

Wanaokabiliwa na keshi hiyo ni Simon Mkina, mhariri mkuu na mmiliki wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa, mhariri, Tundu Lissu, mbunge wa Singida Mashariki na Ismail Mahboob, mchapishaji kutoka kampuni ya Flint

Katika kesi hiyo namba 208 ya mwaka 2016 Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutoa chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.

Patric Mwita wakili wa Serikali Mbele ya Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu amedai kuwa upande wa serikali haujakamilisha maelezo ya awali kwa watuhumiwa hivyo ameiomba mahakama kuja kesho kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo.

Upende wa utetezi uliwakiliswa na Peter Kibatala haukuwa na pingamizi ya ombi hilo.

Awali upande wa Mashtaka ulisoma upya mashtaka mara baada yakushinda pingamizi la utetezi la kutosoma upya mashtaka yaliyofutwa kutokana na kukoseaa kisheria.

Upande wa mashtaka ulisoma shitka la kwanza la la tano kwa kuyarejesha upya kwenye hati ya mashtaka Upande huo ulidai kuwa Shitakala la kwanza ni la kupanga njama za kutoa chapisho la uchochezi, kosa linalodaiwa kutendwa kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka huu ambapo; Idrisa, Mkina na Lissu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam walipanga njama za kuchapisha taarifa za uchochezi.

Katika kosa la tano, mshitakiwa namba moja (Idrissa), namba mbili (Mkina) na namba nne (Lissu), wanatuhumiwa kuchochea hofu miongoni mwa wananchi kwa kuchapisha habari“Machafuko yaja Zanzibar” na kwamba habari hiyo ingeweza kuzua vita au umwagaji damu.

Mashtaka hayo yalikuwa yanapingwa na mawakili wa upande wa utetezi kwa hoja ya kuwa na upongufu wa kisheria ikiwa pamoja na kutokuwa na kibali cha mwendesha mashtaka wa serikali.

Upande wa Jamhuri ulilazimika kusoma shitaka matatu ambalo ni la pili, tatu na nne.

Shitaka pili likimkabili Jabir, Mkina na Lissu, wakidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.

Shitaka la tatu linamuhusu Ismail akidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari ‘Machafuko yaja Z’bar’.

Shitaka la nne linamkabili Ismail akidaiwa kuchapisha gazeti bila kupeleka kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Upande wa Jamhuri umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilka hivyo wameimba Mahakama ipange tarehe ya usikilizwaji wa awali.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Januari, 2017.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

error: Content is protected !!