January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya wafanyabiashara Dodoma yaiva

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya mkoa wa Dodoma imepanga kusikiliza kesi ya wafanyabiashara 95 wenye vibanda 100 wa soko kuu la Majengo, manispaa ya Dodoma ambao wanapinga kubomolewa vibanda vyao katika eneo hilo la soko na Manispaa Dodoma. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Uamuzi huo ulitolewa mbele ya mahakama hiyo na Jaji Makuru wakati alipokuwa akisikiliza maombi ya wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakitaka kusikilizwa kwa kesi yao.

Jaji huyo amesema kuwa maombi ya wafanyabiashara hayo ni ya msingi hivyo mahakama yake imeridhia maombi hayo na imeamua kupanga tarehe ya kusikiliza kesi hiyo namba 117 ya mwaka 2015.

“Mahakama imeridhia maombi ya wafanyabiashara hawa hivyo kesi yao itaanzwa kusikilizwa rasmi Januari 19 mwaka huu,” amesema.

Aidha alibainisha kuwa kutokana na maombi yaliyofikishwa kwake na wakili wa upande wa mashitaka Msomi Machibya ametaka kesi hiyo ambayo ni ya madai isikilizwe na kwamba anakubaliana na maombi hayo.

Kwa upande wao mawakili wa pande zote mbili walieleza mahakama hiyo kuwa wanaridhia tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Hivi karibuni wafanyabiashara hao walipeleka ombi mahakamani zuio la muda kupinga kubomolewa vibanda vyao ambavyo vinadaiwa kuwepo pembeni ya mto pombe uliopo katikati ya soko hilo.

Hata hivyo Manispaa ya Dodoma ilitaka kuvibomoa vibanda hivyo kwa lengo la kuweza kufanya usafi kwenye mto huo licha ya wafanyabiashara hao kujichangisha na kufanya usafi katika mto huo.

error: Content is protected !!