Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya wabunge CUF Agosti 25
Habari za Siasa

Kesi ya wabunge CUF Agosti 25

Wabunge wa CUF wakizungumza na Wakili wao Peter Kibatala walipokuwa katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam
Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam itatoa uamuzi tarehe 25 Agosti mwaka huu, wa pingamizi zilizowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusiana na kesi ya kupinga uteuzi wa wabunge wanane wapya uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoka Chama cha Wananchi (CUF), anaandika Faki Sosi.

Msajili wa Mahakama Kuu, Mustapha Siyani, ameeleza leo kwa niaba ya Jaji Lugano Mwandambo kwamba suala la walalamikaji kuomba amri ya zuio la kuapishwa kwa wabunge wapya mpaka uamuzi utakapotolewa, halina uzito kwa sasa kwa vile Bunge litakapokutana tarehe 5 Septemba uamuzi utakuwa umetolewa.

Ombi hilo lilitolewa na wabunge wanane wa CUF ambao walitangazwa kufukuzwa uanachama Julai 24 mwaka huu, kwa madai ya utovu wa nidhamu na usaliti kwa chama hicho, ikiwemo kudaiwa kumdhalilisha Profesa Ibrahim Lipumba, anayeshikilia uenyekiti kwa kutambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na sio chama.

Profesa Lipumba, aliyejiuzulu kwa hiari yake Agosti 5, 2015, ni miongoni mwa walalamikiwa katika kesi ya msingi Na. 143/2017, akiwa ndiye aliyetoa taarifa ya kuvuliwa uanachama wabunge wanane na madiwani wawili wa Viti Maalum ambao waliteuliwa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

Wabunge hao ni Severine Mwijage, Saumu Heri Sakala, Riziki Shahari Ngwali, Rais Abdalla Mussa, Miza Bakari Haji, Khadija Salum Ali, Halima Ali Mohamed.

Wabunge hao wamefungua kesi iliyoandamana na ombi la zuio la kuapishwa, wakipinga uteuzi wa Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Kiza Mayeye, Zainabu Mndolwa Amir, Hindu Hamis Mwenda, Sonia Magogo, Afredina Kahigi na Nuru Bafadhili.

Waliteuliwa baada ya taarifa za kufukuzwa kwa wabunge kufikishwa kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye naye, baada ya kujiridhisha na taratibu, aliijulisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa zipo nafasi wazi za kujazwa.

Pingamizi zilizowasilishwa na walalamikiwa zinahusu kwamba maombi ya kupinga uteuzi yaliwasilishwa kwa kifungu kisicho sahihi cha sheria. Baada ya Mahakama Kuu kuliondoa ombi hilo kwa kasoro hiyo, wafungua maombi wanaowakilishwa na wakili Peter Kibatala, walirekebisha ombi kwa kuweka kifungu kilicho sahihi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!