Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya Uhujumu uchumi yatua kwa watoa mimba
Habari Mchanganyiko

Kesi ya Uhujumu uchumi yatua kwa watoa mimba

Spread the love

AWADHI Juma, Daktari katika kituo cha afya binafsi cha Dental Clinic, kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam na muuguzi mmoja, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa makosa saba ikiwamo utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 260,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Juma na mshtakiwa wa pili, Kidawa Ramadhani katika kesi namba 139 ya mwaka 2019 pia wanadaiwa kutoa mimba wagonjwa waliingiza bomba la sindano katika uke wa mgonjwa F.R na S.S na kusababisha kuharibika kwa mimba.

Leo tarehe 27 Desemba 2019, Mbele ya Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo,  Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amewasomea washtakiwa hao mashtaka yao.

Awali, Hakimu Mwaikambo amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP.

Miongoni mwa mashtaka hayo, Simon amedai, katika tarehe tofauti Oktoba 2019 eneo la Sinza Mori, jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao wakiwa na lengo la kutoa mimba mgonjwa.

Pia, katika tarehe tofauti, Agosti 2002, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Juma kwa lengo la kudanganya, alighushi cheti cha Diploma cha Utaalam wa tiba ya Kinywa akionesha ni halali na kimetolewa na  chuo cha tiba cha Muhimbili wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la kutakatisha fedha, Juma anadaiwa  kati ya Mei 2015 na Desemba 4, 2019  alijipatia Sh 260,000  wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la jinai la kugushi.

Simon alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Mwaikambo, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2020 itakapotajwa.

Washitakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!