September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Tito Magoti yapigwa kalenda

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, imeahirisha kesi inayomkabili Tito Magoti, mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Magoti, mwingine kwenye kesi hiyo namba 137 ya mwaka 2019 ni Theodory Giyan mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambaye naye ni mtumishi wa LHRC.

Leo Jumatano tarehe 13 Mei 2020, Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Mwaikambo ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 27 Mei 2020, kwa kuwa Hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo tangu awali Hakimu Mkazi Mkuu, Janneth Mtega hakuwepo.

Magoti na mwenzake, walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo tarehe 24 Disemba 2019, na kushtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kushiriki genge la uhalifu kumiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa kwa lengo la kutenda uhalifu na utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 17 milioni.

error: Content is protected !!