Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Sabaya: Shahidi amng’akia Wakili wa Sabaya
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Sabaya: Shahidi amng’akia Wakili wa Sabaya

Lengai ole Sabaya
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Arusha imeelezwa jinsi mshitakiwa wa tatu, Daniel Bura kwenye kesi ya unyang’anyi inayomkabili, pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya alivyotambuliwa na shahidi wa sita, Bakari Msangi kwenye gwaride la utambulisho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Aidha, shahidi wa nane wa Jamhuri, Magdalena Mallya (32) anayefahamika kama Zulfa, amemwonya wakili aache kumwuliza maswali ya kumdhalilisha alipomwuliza, endapo watoto wake amewazaa na mume mmoja au tofauti.

Inspekta wa Polisi, Evarist France Mwamengo (45), alisema hayo juzi Jumatatu tarehe 9 Agosti 2021 akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Omworo anayesikiliza shauri hilo la jinai namba 105/2021 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Arusha.

Aliieleza Mahakama, tarehe 16 Februari 2021, alisimamia gwaride la utambulisho, ambapo shahidi wa sita, Msangi alimtambua mshitakiwa namba tatu, Bura kwa kumwangalia usoni, kisha akazunguka kwa nyuma na kumshika bega.

Shauri hilo lilikuja kwa ajili ya upande wa utetezi kupoitia kwa Wakili Dancun Oola kuuliza maswali ya udadisi kwa shahidi. Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Ndugu shahidi, baada ya kumtafuta kwa muda mrefu yeye alikupigia akakwambia yuko wapi?

Shahidi: Tulia Lodge.

Wakili: Ni kweli kwamba Lodge Hotel na Guest ni tofauti?

Shahidi: Sijui, mana’ke sina mazoea ya kwenda huko.

Wakili: Sema tu hujui. Ulisema wewe ni mwalimu, kiwango chako cha juu ni kipi?

Shahidi: Kidato cha nne.

Wakili: Kiwango chako cha juu cha chuo ni kipi?

Shahidi: Ualimu kiwango cha daraja la tatu.

Wakili: Kwa kiwango hicho cha elimu, unaweza kujua mtu anayeshikiliwa na Sabaya, na aliyetekwa na Sabaya je, kuna tofauti?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Je, baada ya kuachiliwa wakati anaachwa ni kweli kwamba ulikuwa naye?

Shahidi: Nilikuwa naye.

Wakili: Ni wapi mlielekea kwanza, baada ya kuachwa?

Shahidi: Tulikwenda nyumbani.

Wakili: Na ni kweli kwamba simu ya kwanza aliyoipiga ilikuwa ni ya RC?
Shahidi: Hiyo ni simu ya kwanza kupokewa?

Wakili: Ya kwanza ilikuwa ni ipi?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Nyingine aliyopiga ni ipi?

Shahidi: Sijui, alishika simu akapiga, namba ya kwanza akapiga haikupokewa, akapiga nyingine haikupokewa, ila ya kwanza iliyopokewa ni ya RC.

Wakili: Unakumbuka mlikwenda Polisi lini?

Shahidi: Tulikwenda Jumanne, lakini ilikuwa ni zaidi ya saa sita kwa mpango wa saa 24, siku ilikuwa imepita, hivyo ilikuwa ni Jumatano.

Wakili: Unaweza kukumbuka mlikaa Polisi kwa muda gani?

Shahidi: Sikumbuki, alielezea kwa kifupi kisha tukapewa fomu ya PF3?

Wakili: Kwa hiyo maelezo mafupi ya muda gani?

Shahidi: Zaidi ya nusu saa.

Wakili: Zaidi ya nusu saa ni muda mfupi?

Shahidi: Sijui kama kuna siku nyingine aliyotoa maelezo hilo ni swali lake.

Wakili: Unakumbuka wakati unakwenda hospitali mmeshapewa PF3 mlikuwa bado na Feruz (jirani aliyekuwa anaendesha gari)?

Shahidi: Sikupewa PF3 mkononi, mana’ke unasema nilipewa.

Wakili: Unaweza kukumbuka mlikuwa wangapi kwenye gari?

Shahidi: Mimi jirani yangu na Bakari.

Wakili: Kulikuwa na wengine tena?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Ile PF3 aliyopewa Polisi ulishuhudia akiitoa?

Shahidi: PF3 aliibeba OC CID na nilipoiomba kwa daktari sikupewa.

Wakili: Kwa hiyo wewe ndiye uliomba PF3 si Bakari?

Shahidi: Ile PF3 hatukupewa kuipeleka hospitali, wala hatukuirudisha sisi hata alipoiomba hakupewa.

Wakili: Kwa hiyo unaishuhudia Mahakama, kuwa polisi ndio walitoa PF3 na wao ndio waliitoa hospitali.

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Kwa hiyo unaishuhudia Mahakama kuwa polisi waliwahudumia vizuri?
Shahidi: Polisi walitusindikiza wakatufikisha hospitali tukatibiwa na tukaondoka.

Wakili: Mimi nataka kujua Polisi!

Shahidi: Walituhudumia vizuri.

Wakili: Kuna wakati wowote ulishuhudia Sabaya akimpiga Bakari?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Ni hayo tu Mheshimiwa.

Baada ya hapo, Mosses Mahuna ambaye ni Wakili wa mshitakiwa wa kwanza alimhoji shahidi ifuatavyo:

Wakili: Unasema mumeo alikupigia simu saa tano na madakika, unamaanisha nini?

Shahidi: Zaidi ya saa tano usiku.
Wakili: Na dakika 59?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Unamaanisha nini?

Shahidi: Saa tano na dakika 10, 15 au 28.

Wakili: Hiyo simu aliyokupigia unayo?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Umeleta print out za miito kuonesha mume wako alikupigia muda huo?

Shahidi: Sijaleta.

Wakili: Ulichukua muda gani kutoka Sombetini mpaka Tulia Lodge?

Shahidi: Nilimwomba dereva aendeshe gari kasi sana.

Wakili: Ulitumia muda gani?
Shahidi: Sikupima muda.

Wakili: Kwa kawaida ni muda gani kutoka Tulia mpaka nyumbani kwako?

Shahidi: Sijui, kwa sababu sijawahi kwenda Tulia.

Wakili: Nitakuwa sahihi nikikwambia, kwamba hujui muda kuanzia muda uliofika Tulia na gari la Sabaya lilipoondoka?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Hujui muda uliotumika?

Shahidi: Ni kama dakika 10, kwa sababu kulikuwa na muda wa kupokea maelekezo kutoka kwa Mheshimiwa.

Wakili: Kwa hiyo na hizo ni dakika ngapi?

Shahidi: Kwa ujumla ni 10.

1 Comment

  • Duuuuu Sabaya kuendelea kunyea ndooni viongozi mjifuze madaraka ni umepo tuu huwenda ukabadilika kwa kasi ya ajabu kuliko ya kisulisuki. Tz tupo na viongozi wengi wa aina ya sabaya Bashite na wengine wapo ZnZ Pemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!