August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Ndasa yakwama

Spread the love

KESI ya rushwa inayomkabili Richard Ndasa, Mbunge wa Sumve leo imekwama kuendelea kutokana na kutokamilika kwa ushahidi, anaandika Faki Sosi.

Shauri hilo limeahilishwa na Hellen Liwa, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu baada ya upande wa mashitaka kuiombia mahakama kuwa, hawajakamilisha ushahidi wa kesi hiyo.

Ndasa alifikishwa mahakama hapo tarehe 1 Machi mwaka huu kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh. 30 milioni kwa Felichesmi Mramba, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

error: Content is protected !!