July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Minja kusikilizwa mfululizo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, (mwenye koti la kahawia), akisindikizwa na mawakili na wafanyabiashara wenzake

Spread the love

KESI ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara chini, Johnson Minja, imepangwa kusikilizwa siku tatu mfululizo. Aaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Rhada Ngimilanga, ameipiga kalenda kesi hiyo hadi Juni 8 itakaposikilizwa mpaka Juni 10 mwaka huu.

Hata hivyo, amewataka waendesha mashitaka kuwa na mashahidi 15 ambapo wanne wanatakiwa kufika siku ya kwanza ya usikilizwaji wa kesi hiyo wakiwa na wito wa mahakama.

Akisoma maelezo ya awali mbele ya hakimu Mfawidhi, Wakili wa Serikali, Paul Kadushi, amedai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka jana, katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

Amedai kuwa, mshitakiwa anakikabiliwa na mashtaka mawili ya kuwachochea wafanyabiashara wa mkoa wa Dodoma kutenda kosa na kosa la pili ni kuwazuia wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa kutumia mashine za kieletroniki (EFD’s).

Paul amefafanua kuwa, katika kosa la kwanza mshtakiwa alitenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria namba 390 kinachokwenda sambamba na kifungu cha 35 cha kanuni za adhabu sura ya 16.

Katika kosa la pili, mshatakiwa anadaiwa kutenda kosa kinyume na sheria kifungu cha 107(c) cha sheria ya kodi sura ya 332 ya mwaka 2014. Mshitakiwa alikana kutenda makosa yote mawili.

Kama ilivyokuwa siku zilizopita kila kesi hiyo inaposikilizwa, leo pia hali ilikuwa hiyo kwa wafanyabiashara kufunga maduka na kufurika mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya kiongozi wao.

error: Content is protected !!