Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mdee na wenzake rasmi kesho, Kibatala ajipanga kuwahoji
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mdee na wenzake rasmi kesho, Kibatala ajipanga kuwahoji

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajiwa kuanza kusikiliza rasmi shauri la kupinga kuvuliwa uanachama la Halima Mdee na wenzake 18 katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kesho tarehe 26 Agosti 2022 saa nne asubuhi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam …(endelea).

Mdee na wenzake wanaishtaki bodi ya Wadhamini ya Chadema kwa niaba ya Chama hicho, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Awali tarehe 29 Julai mwaka huu Mahakama hiyo ilitoa amri ya wito kwa Halima Mdee na wenzake saba kufika mahakamani hapo tarehe 26 Agosti 2022, kwa ajili ya kuhojiwa na Mawakili wa Chadema.

Jopo la Mawakili wa Chadema liliongozwa na Peter Kibatala mbele ya Jaji Cyprian Mkeha wameiomba Mahakama hiyo Mdee na wenzake kufika mahakamani hapo ili upande huo uwahoji.

Mbali na Mdee wengine walioitwa ni pamoja na Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga, Nusrat Henje, Cecil Pareso, Ester Matiko na Ester Bulaya.

Jaji Mkeha alitoa amri ya wanasiasa hao kufika mahakamani siku hiyo.

Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani

Akizungumza na MwanaHalisi Online Kibatala ameeleza kuwa sehumu ya mahojiano watakayoyafanya na waombaji hao ni kuhusu yale waliyoyaeleza kwenye kiapo chao.

Ameeleza kuwa kwenye kiapo cha wanasiasa hao wameeleza kuwa Chadema kimewateua kihalali kwenda Mahakamani ambapo upande huo utahoji uhalali wao.

Mbali na ombi hilo tarehe 5 Agosti Mawakili wa Chadema waliwasilisha kiapo kinzani dhidi ya kiapo vya waombaji.

Mdee na wenzake wanapinga kufutiwa uanachama wa chama hicho na kuiomba mahakama kupitia mchakato wa kutimuliwa kwao.

Pamoja na kupinga mchakato wameomba mahakamani hiyo kwamba Chadema iwape haki ya kuwasikiliza, kutengua uamuzi wa baraza kuu wa kufukuzwa chamani.

Uamuzi wa Baraza Kuu uliwafanya Mdee na wenzake kukata rufaa iliyosikilizwa tarehe 12 Mei 2022 na Kamati Kuu ya Chama hicho na kupelekea kufukuzwa uanachama wao.

Kwenye kesi hiyo wanasiasa hao 19 wanawakilishwa na jopo la mawakili liliongozwa na Ipioinga Panya, Edson Kilatu, Emmanuel Ukashu, na Aliko Mwamanenge.

Mdee na wenzake wanawashtaki Bodi ya Wadhamini ya Chadema kwa niaba ya Chama hicho, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Taifa (NEC).

Katika kesi hiyo vigogo mbalimbali wa serikali na mhimili wa Bunge wataitwa akiwamo Spika mstaafu, Job Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!