August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mdee, Kubenea yapigwa kalenda

Spread the love
 KESI ya shambulio inayowakabili Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo na Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga imeahirishwa leo katika Mahakama ya Kisutu kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi, anaandika Faki Sosi.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Shafii Juma, mfuasi wa Chadema; Manase Mjema, Diwani wa Kimanga pamoja na Alfonce Kinyafu, Diwani wa Kimara Saranga ambao kwa pamoja wanadaiwa kumshambulia Theresia Mmbando, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa harakati za Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Helleni Liwa, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 2 Juni mwaka huu.
Mdee, Waitara, Shafii na Kinyafu walifikishwa mahakamani hapo tarehe 2 Machi mwaka huu ambapo Kubenea na Mjema wakifikiswa 11 Machi.
error: Content is protected !!