December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mdee hakimu awakia serikali

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashataka kuharakisha ushahidi kwenye kesi inayomkabili Halima Mdee Mbunge wa Kawe ya ya kutumia lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli ili iishe kabla ya mwaka mpya. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo Mahakamani hapo Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba aliyasema hayo baada ya upande Jamhuri kushindwa kumleta shahida.

Kesi hiyo imeahilishwa leo kutokana na kutofika kwa shahidi huyu ambapo Hakimu Simba alipanga kesi hiyo kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, Desemba 10 na 11, wakati mahakama itakaposikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mdee mahakamani Julai 10, 2017 kwa tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Rais.

Inadaiwa kuwa Mdee alifanya kosa hilo tarehe 3 Julai mwaka jana kwenye makao Mkuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Mdee anatuhumiwa kutamka kuwa Rais Magufuli ‘anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki.’

Upande wa mashtaka ishawasilisha mashahidi watatu mahakamani hapo.

error: Content is protected !!