December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe yaahirishwa hadi J3, Jaji asema…

Spread the love

 

JOACHIM Tiganga, Jaji anayesikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, ameiahirisha hadi Jumatatu, tarehe 22 Novemba 2021, ili kutoa uamuzi mdogo wa pingamizi la utetezi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pingamzi hilo, liliwekwa jana Jumatano, tarehe 17 Novemba 2021, wakipinga barua iliyowasilishwa na shahidi wa pili wa Jamhuri, Ricardo Msemwa kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka isipokelewe kama kielelezo.

Mawakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya na Peter Kibatala walitoa hoja wakipinga suala hilo kwamba barua hiyo ilikwisha kutolewa uamuzi mahakamani hapo kwenye kesi ndogo iliyohusu maelezo ya onyo ya Adam Kasekwa.

Mawakili hai, waliweka pingamizi hilo wakati shahidi huyo wa pili wa Jamhuri ambaye ni askari polisi, Ricardo Msemwa akitoa ushahidi kwenye kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo wa mshtakiwa, Mohamed Ling’wenya yasipokelewe kwa kile walichodai hakuyatoa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam wala Kituo cha Polisi Mbweni jijini humo.

Mawakili wa utetezi walitoa hoja zao na ikafuatia wa mashtaka kuzijibu na sasa mawakili tena wa utetezi wanajibu hoja zilizoibuliwa na mashtaka.

Mbali na Mbowe, Ling’wenya na Kasekwa mwingine ni Halfan Hassan Bwire ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makossa ya kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.

Mara baada ya mawakili wa pande zote walioanza kujenga hoja jana na kumaliza leo, Jaji Joachim Tiganga aliahirisha kwa muda ili kwenda kufikiria ni lini hasa atatoa uamuzi huo.

Baada ya kurejea, Jaji Tiganga amesema, kesho Ijumaa haiwezekani hivyo atatoa uamuzi huo Jumatatu huku mawakili wa pande zote wakikubali.

error: Content is protected !!