Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe, wenzake; Mke wa mshtakiwa aanza kutoa ushahidi, walivunja mlango!
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe, wenzake; Mke wa mshtakiwa aanza kutoa ushahidi, walivunja mlango!

Spread the love

 

MKE wa mshtakiwa Adam Kasekwa ambaye ni shahidi wa tatu wa utetezi, Lilian Kibona, ameanza kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Uhujumu Uchumi, kwenye kesi ndogo ndani ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Shahidi huyo ameanza kutoa ushahidi wake leo Jumatano, tarehe 29 Septemba 2021 katika mahakama hiyo, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Kibona ameieleza mahakama hiyo kuwa, yeye na mume wake walifunga ndoa mwaka 2016 na kubahatika kupata mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na miezi tisa.

Akiongozwa na Wakili John Mallya, amedai kabla mume wake hajaenda Moshi mkoani Kilimanjaro, aliwasiliana na mshtakiwa mwenzake, Mohammed Abdillah Ling’wenya, ambapo alimwambia kuna kazi hivyo waende wakaifanye mkoani humo.

Amedai, baada ya mume wake kupigiwa simu hiyo, walisafiri na Ling’wenya kuelekea Morogoro kisha akarudi nyumbani kwao Chalinze mkoani Pwani kwa ajili ya kujipanga kwa safari.

Kibona amedai, baadae mume wake na Ling’wenya walisafiri kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo asubuhi ya tarehe 5 Agosti 2020 alimpigia simu kwa ajili ya kumjulia hali lakini akakatisha mawasiliano na kumwambia atampigia baadae.

Amedai hadi majira ya jioni mume wake hakumpigia simu, kama alivyomuahidi na kuamua kumpigia tena lakini simu yake iliita kisha kupokewa bila ya mtu kuongea.

Kibona amedai, baadaye alimpigia Ling’wenya, ambaye simu yake iliita kuanzia jioni hadi kesho yake asubuhi ndipo ikazimwa.

Polisi wavunja mlango

Wakili Mallya alipomuuliza anakumbuka tukio gani lililotokea Jumapili ya tarehe 9 Agosti 2020, Kibona alijibu akidai, alipokuwa anarudi kutoka hospitalini alikompeleka mwanaye kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na tumbo, alikuta alama za miguu ya watu mlangoni kwake huku ukiwa wazi ilhali aliufunga.

Amedai, katika nyumba yao hiyo iliyopo maeneo ya Lamboni, Chalinze mkoani Pwani, alikuta kitasa cha mlango wake kimevunjwa, akaingia ndani na kuangalia vitu vya harakaharaka ikiwemo televisheni kama vipo, ambapo alivikuta viko salama.

Amedai, alipoingia hadi chumbani alikuta nguo za mume wake zimemwaga, huku begi lake la kijeshi alilonunua akiwa nchini Congo, halipo.

Pia, amedai watu hao walichukua vyeti vya kijeshi vya Kasekwa, hati ya Kiwanja na kadi ya pikipiki.

Mke wa mshtakiwa huyo amedai, baada ya kuona tukio hilo, alikwenda kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Eunice Charles, kumuuliza nini kilitokea, ambapo alimwambia kuna magari ya polisi yalifika nyumbani kwake, huku baadhi ya polisi wakiwa wamevaa kiraia na wengine sare.

Amedai, jirani yake huyo alimpatia mawasilinao ya Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Chalinze, mkoani Pwani, ili kama kuna jambo lolote ampigie amuulize.

Kibona amedai, baada ya kumpigia simu mkuu huyo wa upelelezi, alimwambia alipigiwa simu kutoka Jeshi la Polisi Moshi, iliyomuelekeza kufanya upekuzi nyumbani kwa Adam Kasekwa, ambaye ni mume wake.

Kasekwa na mshtakiwa mwenzake, Mohammed Abdillah Ling’wenya, walikamatwa na Jeshi la Polisi, maeneo ya Rau Madukani, Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 5 Agosti 2020, kwa kosa la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi.

Kesi hiyo ndogo katika kesi inayowakabili washtakiwa hao na Halfan Bwire Hassan, imetokana na pingamizi la utetezi dhidi ya maelezo ya onyo ya Kasekwa, wakipinga yasitumike mahakamani hapo kama ushahidi wa jamhuri wakidai yalichukuliwa kinyume cha sheria.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!