December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe wanavyochuana kortini

Spread the love

 

MAWAKILI wa pande mbili katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wanachuana katika pingamizi la utetezi dhidi ya barua iliyowasilishwa mahakamani hapo na shahidi wa pili wa jamhuri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo wa mshtakiwa, Mohamed Ling’wenya yasipokelewe kwa kile walichodai hakuyatoa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam wala Kituo cha Polisi Mbweni jijini humo.

Pingamizi hilo, limeanza kusikilizwa jana Jumatano na linaendelea leo Alhamisi, tarehe 18 Novemba 2021 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Mawakili wa utetezi, wamedai barua hiyo ya shahidi, ambaye askari polisi, Ricardo Msemwa isipokelewe kwani imewahi kutolewa uamuzi wa barua hiyo kwenye kesi ndogo ya kupinga maelezo ya Adam Kasekwa yasipokelewe.

Mawakili wa utetezi walitoa hoja zao na ikafuatia wa mashtaka kuzijibu na sasa mawakili tena wa utetezi wanajibu hoja zilizoibuliwa na mashtaka.

Mbali na Mbowe, Ling’wenya na Kasekwa mwingine ni Halfan Hassan Bwire ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makossa ya kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!