November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Shahidi aeleza uchunguzi bastola ulivyofanyika

Spread the love

 

SHAHIDI wa tatu wa Jamhuri, Koplo Hafidhi Abdllah Mohammed, katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe, ameeleza namna alivyofanya uchunguzi wa silaha ‘bastola’  inayodaiwa kuwa alikamatwa nayo mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adam Kasekwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Koplo Hafidhi ameelezea uchunguzi huo leo Ijumaa, tarehe 29 Oktoba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, Koplo Hafidhi amedai, tarehe 25 Novemba 2020 alipokea vielelezi kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), ambavyo nisilaha aina ya Pisto, magazini na risasi tatu za Pisto. Ambapo barua ya vielelzo hivyo ililetwa na mtu aliyemtaja kwa jina la  Goodluck.

Mtaalamu wa masuala ya uchunguzi wa silaha na milipuko, katika kitengo cha Matumizi ya silaha na milipuko, amedai barua hiyo ilimuelekeza achunguze vielelezo hivyo kama ni vizima, ambapo tarehe 25 Novemba 2020 alivifanyia uchunguzi wa awali.

Koplo Hafidhi amedai, alipochunguza ile Pisto alibaini inafanya kazi.

Koplo Hafidhi amedai, baada ya kuvifanyia uchunguzi wa awali wa Pisto hiyo, alifanya uchunguzi wa kina wa risasi alizokabidhiwa alibaini kuwa vinafanya kazi.

Koplo Hafidh amedai, ripoti ya uchunguzi wa vielelzo hivyo, aliikabidhi kwa Afande Swila kutoka Ofisi ya DCI.

Baada ya kutoa ushahidi huo, Wakili Hilla alimuuliza  Koplo Hafidhi anaiomba nini mahakama hiyo, ambapo alijibu akidai anaiomba ipokee ripoti ya uchunguzi huo kama sehemu ya ushahidi wake.

Baada ya kutoa maombi hayo, Jaji Tiganga aliuuliza upande wa utetezi kama una mapingamizi dhidi yake, ambao ulijibu ukidai hakuna.

Jaji Tiganga aliipokea ripoti hiyo ya uchunguzi kama kielelezo namba mbili cha upande wa mashtaka katika kesi hiyo.

Vielelezo hivyo vinadaiwa kuwa alikamatwa navyo Kasekwa, tarehe 25 Agosti 2020, maeneo ya Rau Madukani, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mbali na shtaka la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi katika kesi hiyo, Kasekwa anadaiwa kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya Pistol na risasi tatu, vifaa vinavyodaiwa kuwa alipanga kuvitumia katika vitendo vya ugaidi.

Sehemu ya mahojiano yake na wakili wa serikali;

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama mnamo tarehe 25 Novemba unakumbuka ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa ofisini kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi?

Shahidi: Kwenye dawati la kupokea vielelezo mbalimbali.

Wakili wa Serikali: Ulipokea vielelezo vipi siku hiyo?

Shahidi: Nilipokea vielelezo kutoka Ofisi ya DCI ambavyo ni pistol yenye namba A5340 caliber 9mm ikiwa na magazine yenye rangi nyeusi na nikapokea risasi tatu.

Wakili wa Serikali: Za silaha gani?

Shahidi: Za _pistol caliber 9mm.

Wakili wa Serikali: Vielelezo hivyo viliambatana na nini?

Shahidi: Kwanza alivileta PC Goodluck kutoka Ofisi ya DCI.

Wakili wa Serikali: Goodluck aliwasilisha nini?

Shahidi: Barua.

Wakili wa Serikali: Baada ya kupokea vielelezo hivi na barua ieleze Mahakama ulifanya nini.

Shahidi: Nilivi- label kama nilivyosema awali. Pistol niliipa alama Exhibit K1 … Ni kosa ili kwa FB /BALL/LAB 158/2020.

Wakili wa Serikali: Na hizi risasi tatu?

Shahidi: Nilizipa alama ya K2 K3 na K4.

Wakili wa Serikali: Risasi hizi ulizipa usajili upi?

Shahidi: 158 kama pistol

Wakili wa Serikali: Baada ya kukamilisha usajili wa vielelezo ulichukua hatua gani?

Shahidi: Nikarudi kwenye barua kujiridhisha wanataka nini wafanyiwe.

Wakili wa Serikali: Sawa. Ukibaini wanataka kitu gani?

Shahidi: Kufanya uchunguzi wa kuutambua hiyo bunduki na risasi ni nzima K2, K3 na K4.

Wakili wa Serikali: Na kuhusu vielelezo pistol na risasi ukafanya nini?

Shahidi: Kwanza ile pistol niliipima.

Wakili wa Serikali: Kabla ya kupima, tupo kwenye hatua ya upokeaji.

Shahidi: Nika- minutes kumpelekea Boss.

Wakili wa Serikali: Vielelezo ukapeleka wapi?

Shahidi: Nilipeleka chumba cha kuhifadhia silaha.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama nani aliteuliwa kufanya uchunguzi.

Shahidi: Mimi mmojawapo.

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni lini ulipopewa jukumu hilo?

Shahidi: Ilikuwa tarehe 25 Novemba mwaka 2020.

Wakili wa Serikali: Katika uchunguzi huo ulifanya lini?

Shahidi: Nilianza kufanya tarehe 25 uchunguzi wa awali.

Wakili wa Serikali: Katika uchunguzi wako ulifanya nini kulingana na mahitaji?

Shahidi: Hatua ya kwanza.

Wakili wa Serikali: Mteja alikuwa anataka nini?

Shahidi: Mteja alikuwa anataka kujua ile pistol na risasi zilifanya kazi?

Wakili wa Serikali: Sasa wewe ulifanya nini?

Shahidi: Kwanza Ile bastola nilipima na kifaa kinaitwa Gun Barrow Gauge. Hapo nilikuwa napima kwenye barrow,  yaani mtutu, kwamba ile caliber ni kweli 9mm. Nikaona ni kweli ipo sahihi ni 9mm.

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Nikatoa magazine. Kumbuka ilikuwa na magazine inaitwa Magazine Release. Naangalia magazine yake ile bastola ni ya kwake? Nikaona OK, magazine ni ya kwake.

Wakili wa Serikali: Jingine?

Shahidi: Ndani ya magazine kuna spring ambayo ukiweka  risasi inashuka chini. Yenyewe inapandisha risasi juu.  Nikaona ni nzima. Nikaangalia nyundo, hummer, kama ni nzima. Sometime inakuwa loose. Nikabaini ni nzima.

Shahidi: Nikaangalia triger kwa kutumia triger pull kama inafika kwenye 100, nikabaini ni nzima.  Nikai- koki ili nijiridhishe kama inaenda vizuri. Nikaona inaenda vizuri kwenye njia zake na inaenda intact.

Nikaenda ndani ya barrow nikatumia mdeki kuangalia kama ilikuwa Safi au chafu kupoteza ubora wake. Nikabaini _barrow lipo vizuri halina vumbi, hakuna mchanga maana yake barrow lipo safi.  Lolote linaweza kufanya. Baada ya hapo nikaikoki kungalia firing pin mechanism kama ipo. Nilibaini ipo. Kwa hatua hiyo niliishia hapo.

Wakili wa Serikali: Kwa aina za uchunguzi ulizotutajia huu ni uchunguzi wa aina gani?

Shahidi: Ni Visual Examination.

Wakili wa Serikali: Kwenye zile  risasi tatu ulichunguza nini?

Shahidi: Pale niliingia sana kwenye pin impresion kwa maana primer au Kiswahili chake ni kiwashio au kitako cha risasi.

Wakili wa Serikali: Ulibaini nini?

Shahidi: Nilikuwa naangalia risasi nilizoletewa ni nzima. Nilibaini ni nzima.

Wakili wa Serikali: Hatua gani ikafuata?

Shahidi: Hatua ya pili ya uchunguzi wa pili.

Wakili wa Serikali: Kivipi?

Shahidi: Nilichukua risasi mbili ya zile nilizoletewa calibre yake ni 9mm. Nikaenda kwenye chumba maalumu. Kwenye chumba kuna sehemu ya kupigia silaha mbalimbali.

Wakili wa Serikali: Ulienda na kitu gani?

Shahidi: Nilikuwa na Pistol na risasi tatu.

Wakili wa Serikali: Ulienda kufanya kitu gani hasa?

Shahidi: Kuna kifaa kinaitwa Tank Water Recovered Bullets.

Wakili wa Serikali: Kiswahili ni nini?

Shahidi: Ni tanki la maji tunalotumia kupata risasi. Mle kwenye tanki kuna nyavu na kisha tunajaza maji, na unalifunga na kisha anaenda kupiga risasi yako.

Wakili wa Serikali: Kwanini sasa mnapiga risasi kwenye tanki la maji?

Shahidi: Ili kupata  maganda ya risasi na vichwa vyake.

Wakili wa Serikali: Kwanini sasa mnapiga vile vielelezo?

Shahidi: Najiridhisha sasa. Je. ni kweli zile risasi ni nzima? Nakwenda kupiga sasa.

Wakili wa Serikali: Nini matokeo ya uchunguzi wa kina?

Shahidi: Nikichukua risasi mbili nikaweka kwenye magazine. Nikaweka kwenye ile bastola nikapiga sasa. Nikapata  maganda na vichwa vya risasi. Nikafanya hivyo tena kwa risasi ya pili. Nikapiga.

Wakili wa Serikali: Risasi zako zilikuwa na alama. Je, risasi za alama zipi ambazo ulipiga?

Shahidi: K2 na K4

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini sasa kuhusiana na yale maganda?

Shahidi: Nilienda kuya- label yale maganda yangu mawili.

Wakili wa Serikali: Kwa kuyapa alama gani?

Shahidi: T1 na T2. T1 ilikuwa K2 na T2 iliyokuwa K4.

Wakili wa Serikali: Baada ya labelling ni kitu gani sasa kingine kilifuata?

Shahidi: Nikaenda kuandaa riport yangu (Ballistic Examination Report).

Wakili wa Serikali: Baada ya kuandaa ulifanya nini?

Shahidi: Nilisaini.

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Nilipiga muhuri.

Wakili wa Serikali: Muhuri gani?

Shahidi: Forensic Bureau Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Kuhusiana sasa na silaha yenyewe.

Shahidi: Baada ya hatua zote zote hizo nikafunga kwenye mfuko na nikafunga seal, nikasaini na kuandika tarehe.

Wakili wa Serikali: Baada ya kusaini ukapeleka wapi?

Shahidi: Chumba cha kutunzia silaha.

Wakili wa Serikali: Na report yako sasa?

Shahidi: Niliweka kwenye bahasa na nikairudisha kwenye file Book. Baada ya hapo nikiwa nasubiri wenyewe waje kuchukua vielelezo vyao.

Wakili wa Serikali: Vielelezo vyao vilikuwa vilichukuliwa siku gani?

Shahidi: Tarehe 27 Novemba 2020.

Wakili wa Serikali: Nani alikuja kuchukua vielelezo hivyo?

Shahidi: Afande Swila kutoka ofisi ya DCI.

Wakili wa Serikali: Nani aliyemkabidhi afande Swila hivyo vielelezo?

Shahidi: Mimi mwenyewe.

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Swila vitu gani?

Shahidi: Riport yangu ya kiuchunguzi Ballistic Examination Report. Nikamkabidhi pistol moja ambayo ni Exibit K1 Calibre A5340 9mm. Model yake CZ 41 rangi nyeusi ikiwa na  magazine yake.

Pia nikamkabidhi risasi moja nzima iliyobaki ambayo nilii- label K3.  Nikamkabidhi maganda mawili na bullets zake. Yale maganda niliya- label kama T1 na T2.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama kwamba tangu ulivyomkabidhi Swila ni lini tena ulipata kuviona tena vielelezo?

Shahidi: Jana.

Wakili wa Serikali: Kwa jambo lipi?

Shahidi: Ili aniletee vielelezo kwa ajili ya ushahidi Mahakamani hii leo.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama hii report yako ya kiuchunguzi uliyoiandaa ni kitu gani kitakutambulisha?

Shahidi: Kwanza kwa nembo ya ofisi, nembo ya Polisi. Force namba zangu F5914 na majina yangu ya Koplo Hafidh Abdallah.

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Na signature yangu. Na muhuri wa ofisi.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji shahidi anaonesha anaweza akutambua nyaraka aliyofanyia kazi kwa ruhusa ya Mahakama. Tunaomba kumuonyesha.

(Shahidi anakabidhiwa)

Wakili wa Serikali: Shahidi litizame hilo kabrasha ndogo sasa uimbie Mahakama nilichokupatia ni kitu gani.

Shahidi: Ni report yangu niliyoindaa kuhusiana na uchunguzi wa silaha na risasi.

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama vitu gani vinaonyesha wewe ndiyo uliandaa.

Shahidi: Kuna nembo ya polisi, Force Namba, signature yangu. Kuna muhuri wa ofisi. Kwa hiyo ripoti hii ni ya kwangu.

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama hii?

Shahidi: Naomba Mahakama hii ipokee ripoti yangu kama sehemu ya  ushahidi.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji shahidi anaomba ipokelewa Ballistic Examination Report.

(Wakili wa Serikali anaipeleka upande wa mawakili wa utetezi).

Wakili Nashon Nkungu: Kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza sina pingamizi.

Wakili John Mallya: Kwa niaba ya mshitakiwa wa pili sina pingamizi.

Wakili Dickson Matata: Kwa niaba ya mshitakiwa wa tatu pia hatuna pingamizi.

Wakili Peter Kibatala: Kwa niaba ya mashitakiwa wa nne pia hatuna pingamizi.

(Jaji anapelekewa nyaraka).

(Mahakama bado imekaa kimya kidogo wakati Jaji akiandika).

Jaji: Mahakama imepokea nyaraka hii yenye kichwa cha habari Ballistic Report.

Jaji: Mahakama imepokea nyaraka hii ambayo iliandaliwa tarehe 26 Novemba 2020. Napokea kama kielelezo namba 02.

Jaji: Nakuomba shahidi usaidie kuisoma.

(Shahidi anapewa aisome)

Shahidi: Forensic Bureau Ballistic Laboratory DSM/F ya tarehe 26 Novemba 2020.

(Kisha shahidi anaisoma upya yote)

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

error: Content is protected !!