May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Serikali kutumia mashahidi 24, vielelezo 19

Freeman Mbowe akiwasili mahakamani Kisutu

Spread the love

 

UPANDE wa mashtaka katika kesi inayomkabili Kiongozi wa chama kikuu kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu umepanga kutumia mashahidi 24 na vielelezo vya maandishi 19. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake watatu, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya wamesomewa maelezo ya awali ya tuhuma zinazowakabili ya uhujumu uchumi na kupanga njama za ugaidi leo Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Thomas Simba kwamba watatumia mashahidi 24 na vilelezo vya maandishi 19 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

Amesema, miongoni mwa mashahidi ni wanasheria wa kampuni za simu za Tigo na Airtel ambao waliotoa taarifa za miamala ya fedha kutoka kwa Mbowe kwenda kwa watu wakiwemo washtakiwa wenzake.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!