Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya Mbowe: Pingamizi la Serikali latupwa
Habari Mchanganyiko

Kesi ya Mbowe: Pingamizi la Serikali latupwa

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhumuku Uchumi, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, imetupilia mbali pingamizi la jamhuri la kutaka nyaraka nne za upande wa utetezi zisipokelewe kama kielelezo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Nyaraka hizo ziliwasilishwa jana Jumatatu, tarehe 29 Novemba 2021 na shahidi wa utetezi, Lembrus Mchome wakati akitoa ushahidi wake, katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kesi hiyo ndogo inahusu kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu, Mohammed Abdillah Ling’wenya, yasipokelewe kama kilelezo wakidai, hakuwahi hakuwahi kuyatoa bali alilazimishwa kuyasaini.

Uamuzi wa pingamizi hilo, umetolewa leo Jumanne, tarehe 30 Novemba 2021, na mahakama hiyo mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Akitoa uamuzi madogo dhidi ya pingamizi la upande wa jamhuri, wakiomba nyaraka hizo zilizotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Kilimanjaro, Lembrus Mchome, zisipokelewe, ukidai shahidi huyo hakufuata sheria.

Nyaraka hizo ni, barua ya Wakili Peter Kibatala, kwenda kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba mwenendo wa kesi ya matumizi mabaya ya mitandao, iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo, nyaraka yenye taarifa za mwenendo wa kesi hiyo, dispatch (kitabu cha kuthibitisha upokelewaji wa nyaraka) na hati ya mshtaka.

Jaji Tiganga amesema mahakama hiyo imepokea nyaraka hizo, ili kuokoa muda kwa shahidi aliyezitoa kuwa na tatizo la kiafya, pia nyaraka hizo zitaishia kutumika katika kesi hiyo ndogo.

Mchome ambaye amekuja mahakamani huku akiwa amefungwa mkono wake wa kushoto, anadaiwa kuwa alipata ajali akiwa safarini kuelekea Dar ea Salaam, kuja katika kesi hiyo.

“Mahakama hii kwa kuzingatia kwamba vinalenga kutolewa katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na baada ya hapo vitaishia hapo. Msimamo wa sheria baada ya kuzingatia ukweli jana imeelezwa offline shahidi ana tatizo la kiafya, baada ya kuzingatia upokelewaji vielelezo mahakamani huzingatia vigezo vya awali vya upokelewaji vielezo. Pia, pande zote mbili kubaki na haki ya kuonesha udhaifu wakati wanauliza maswali na mahakama ina haki ya kuchunguza uzito wake,” amesema Jaji Tiganga.

Jaji Tiganga amesema, barua inapokelewa kama kielelezo namba mbili, wakati dispatch ikipokelewa kama kielelezo namba 3, nakala ya hati ya mashtaka (4) na nyaraka yenye taarifa za mwenendo wa kesi (5).

“Mahakama inapokea huku ikijiachia nafasi ya kuchunguza wakati huo itazingatia hoja za pande zote mbili na itatoa uamuzi wa uzito wa vilelezo hivyo,” amesema Jaji Tiganga.

Mchome aliomba mahakama hiyo izipokee nyaraka hizo, alizodai zinathibitisha kuwa aliwekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, tarehe 14 Mei 2020, baada ya kukamatwa mkoani Kilimanjaro, kwa kosa la kupiga picha gari la kiongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Mwenyekiti huyo wa Bavicha Kilimanjaro, alitoa ushahidi uliodai kwamba, aliyekuwa shahidi wa jamhuri, Askari Mpelelezi Msemwa, 2020 hakufanya kazi katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, kama alivyodai wakati anatoa ushahidi wake ya kwamba, tarehe 7 Agosti 2020, aliwapokea wenzake Mbowe, Ling’wenya na Kasekwa, katika chumba cha mashtaka cha kituo hiko.

Mchome alidai kuwa, ushahidi huo uliotolewa na Askari Msemwa si wa kweli, kwani kipindi hiko alikuwa Kituo cha Polisi Oysterbay, kwani yeye ndiye aliyempokea kituoni hapo na kuandika maelezo yake katika kitabu cha mahabusu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!