Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kesi ya Mbowe ni ya kubumba?
Makala & Uchambuzi

Kesi ya Mbowe ni ya kubumba?

Freeman Mbowe akiwasili mahakamani Kisutu
Spread the love

 

HATI ya mashitaka – Charge Sheet – yaweza kukosa uhalali wa kisheria, ikiwa Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DPP), atashidwa kuandaa na kuwa na ushahidi wa kutosha katika kesi anayosimamia. Anaandika Mwanasheria Ester Daffi … (endelea).

Mkurugenzi wa mashitaka anaowajibu mkubwa wa kisheria katika kuandaa na kuendesha mashitaka ya jinai, kama mshitaki wa umma (Public Prosecutor). Anapaswa kujiridhisha kuwa katika shauri analolifungua, ana ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mtuhumiwa.

Haya anapaswa kujiridhisha nayo, kabla ya kufungua kesi mahakamani, na kwamba mashitaka anayofungua yamebeba maslai ya umma (Public Interest).

Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali, anawajibu wa kuhakikisha serikali haipotezi fedha za umma (Public Funds), kwa kupeleka mashitaka ya kubumba na yasiyo kuwa na tija.

Aidha, mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya jinai, anawajibu wa kuionyesha mahakama kuwapo kwa viashiria vya kosa linalodaiwa kutendeka.

Miongoni mwa misingi ya kwanza ya uhalali wa kesi husika, upo kwenye hati ya mashitaka. Hati ya mashitaka inaagua mwenendo mzima wa taratibu za kijinai na mwenendo wa usikilizwsaji – Criminal Court Procedures and Proceedings.

Sylivester Mwakitalu

Msingi mkuu wa hati ya mashitaka ni lazima uwe na mambo yafuatayo. Ni lazima uonyeshe kosa lililotendwa – the tittle of the offence.

Kwa mfano, kama mtuhumiwa anadaiwa kufanya kosa la wizi, ni lazima mkurugenzi wa mashitaka aonyeshe nani ameibiwa au alitaka kuibiwa; na hata kilichotaka kuibiwa kipo au kimeibwa!

Mathalani, hati ya mashitaka ikisema kuna viongozi wa serikali zaidi ya mmoja walitaka kuuliwa, ni lazima iwataje viongozi hao waliotaka kuuliwa.

Ofisi ya mwendesha mashitaka inapaswa kuonyesha lini na wapi, tendo hilo lilitaka kutokea na kwa ushahidi usio na shaka.

yaani circumstances of and harm caused to the victim, wa kuathirika kwa wahanga wa matukio hayo.

Kwamba, kama mshitakiwa anashutumiwa kwa kosa la wizi, hati ya mashitaka lazima ionyeshe ni kitu gani au mali gani mtuhumiwa aliiba kutoka kwa mmiliki halali (lawful owner) na akiwa na nina ovu (dishonest intention) ya kujitwalia au kumiliki mali husika.

Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)

Nitoe mfano wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Mwanasiasa huyo wa upinzani na mbunge wa zamani wa Hai, mkoani Kilimanjaro, anayetuhumiwa kwa makosa ya kupanga njama za ugaidi na kufadhili ugaidi, ikiwamo kulipua vituo vya mafuta na kuuwa viongozi wa serikali.

Kwamba, anayetajwa kutaka kuuawa, ni aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya.

Lakini ndani ya hati ya mashitaka, hakuna ambako kunaonyesha, ni nani wamiliki wa vituo hivyo na mahali ambako vituo hivyo vipo. Hakuna mlalamikaji na wala Sabaya ambaye alipaswa kuwa shahidi muhimu wa upande wa mashitaka, hajaorodheshwa katika orodha ya mashahidi wa upande wa mashitaka.

Kwa maoni yangu, Sabaya alipaswa kuwamo katika orodha ya mashahidi wa upande wa mashitaka – kama kweli mkurugenzi wa mashitaka anaamini kuwa kulikuwa na njama za kutaka kumdhuru mkuu huyo wa zamani wa wilaya.

Wala hati ya mashitaka dhidi ya Mbowe, haisemi lini shambulio hilo lilipangwa kufanyika na kwa njia gani. Haielezi vituo vya mafuta vimeshalipuliwa au bado – yaani very strange speculative charge!

Mahakama inayosikiliza kesi husika, lazima ijiridhishe kuwa makosa anayotuhumiwa nayo mhusika yanakidhi matakwa ya sheria.

Hili ni muhumu kwa kuwa mahakama inapaswa kusaidiwa katika kutoa uwanda sawa wa utetezi kwa mtuhumiwa kwa kuwasilishwa ushahidi usio na mawaa kutoka upande wa washitaki (DPP).

Aidha, hati ya mashitaka ni lazima ioneshe kama mtuhumiwa aliwahi kutiwa hatiani kwa makosa ambayo anashitakiwa nayo wakati huu ambapo amefunguliwa kesi mpya (prior conviction), ili kuisaidia mahakama kufahamu historia ya kijinai ya mtuhumiwa.

Kwa kufanya hivyo, mahakama inakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa hukumu inayostahili kulingana na makosa aliyotenda mtuhumiwa na kuisaidia kuharakisha usikilizwaji wa mwenendo wa kesi yake.

Vilevile, hati ya mashitaka lazima ioneshe sheria na vipengele vya sheria ambapo mashitaka ya mtuhumiwa yanahusika nayo. Hii ni sehemu ya haki ya kisheria ya mtuhumiwa kujua sheria ipi na vifungu vyake vinavyomtuhumu kutokana na mashitaka yanayomkabili, ili kumpa nafasi yake isiyohamishika ya utetezi mbele ya mahakama ya kisheria.

Hati ya mashitaka isiyokidhi matakwa ya kilazima juu ya ufunguzi wa kesi husika, ni sawa na kuwa na kesi hewa na hivyo hakuna kesi ya kujibu.

Kumbuka upande wa mashitaka huwa kila aina ya mahitaji katika kufanya uchunguzi na sasa ina General Solicitor – wakili mkuu wa serikali – ambaye kazi yake ni pamoja kushiriki kuandaa kesi zote za jinai na kuwasilisha utetezi wake mahakamani akishirikiana na DPP.

Itasikitisha kuona ofisi zote hizi na vitendea kazi vyote walivyonavyo, bado Jamhuri inaweza kuja na hati ya mashitaka iliyosheheni matundu.

Hakuna ya namna mkurugenzi wa mashitaka inakosa au kushindwa kufuata misingi ya kisheria niliyotaja hapo juu ili kuwezesha kufungua kesi ya msingi na sio ya kubumba na kuletea serikali hasara katika uendeshaji wa kesi.

Kutaka kuumiza upande wa mshtakiwa au washtakiwa kukaa mahabusu au gerezani na mwishowe mkurugenzi wa mashitaka anakosa ushahidi wa kesi hiyo na hivyo kuamua kuindoa, ni jambo ambalo kinyume cha taratibu.

Kisheria wanaweza kutoka ikiwa waanze upya au wafute mashitaka kabisa hii ni aibu kubwa kwa ofisi ambayo inahusika na makosa yenye maslahi na umma (Interest Publicae).

Haya ni mambo muhumu sana kuonyesha au kutendwa na waendesha mashitaka wetu. Nje ya hapo, watakuwa wanatengeneza kesi ambazo mwisho wa siku watashindwa kuzithibitisha mahakamani.

Hayo yakitokea watakuwa wanaonyesha udhaifu wa kiwango cha juu kwa wasomi wetu katika ofisi ya mwendesha mashitaka.

Mwandishi wa makala haya, Ester Daffi, amejitambulisha kuwa ni mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyepo makao makuu, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam.

1 Comment

  • Asante sana kwa ufanunuzi wa kisheria.

    Tunaomba mtuletee na makala kutoka kwa wakili wa upande wa mleta maombi ya kesi. Endapo itawezekana.

    Rafiki yako,

    Aliko Musa.

    Mbobezi Kwenye Ardhi Na Majengo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!