October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe, Matiko kuanza kusikilizwa kesho

Freeman Mbowe na Ester Matiko wakipelekwa gerezani

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imepanga kusikiliza shauri la madai ya kufutiwa dhamana lililofunguliwa mahakamani hapo na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, kesho Alhamisi asubuhi. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Akighairisha usikilizaji huo kutoka leo hadi kesho, Jaji Sam Rumanyika ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kesi hiyo kusikilizwa kwa haraka.

“Nataka shauri hili lisikilizwe haraka kama ambavyo waombaji walivyoleta maombi yao,” ameeleza Jaji Rumanyika.

Amesema, “mahakama hii, ni sharti izingatie ukweli kuwa kesi hii, imefungukiwa kwa hati ya dharura sana. Hivyo basi, hatuwezi kuacha kusikiliza kesi hii kwa sababu itakuwa inakwenda kinyume na maombi yaliyoletwa.”

Kauli ya Jaji Rumanyika ilikuja kufuatia maombi ya upande wa mashitaka kutaka kesi hiyo isikilizwe Jumatatu ijayo.

Akiwasilisha maombi hayo mahakamani, wakili mkuu wa serikali, Faraja Nchimbi, alidai kuwa upande wa mashitaka hauko tayari kuendelea kesi hiyo, hadi itakapopewa mwenendo mzima wa kesi.

IMG-20181128-WA0032

Akijibu madai hayo, Jaji Rumanyikwa aliagiza kesi hiyo kusikilizwa kwa kutumia mwenendo wa kesi ambao haujachapwa ili kulinda haki za waomba rufaa.

Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana tarehe 23 Novemba mwaka huu, kufuatia madai ya kuidharau mahakama na kukiuka masharti ya dhamana.

error: Content is protected !!