May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe kusikilizwa kimtandao akiwa gerezani

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, inasikiliza kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe kwa njia ya mtandao ‘Video Conference.’ Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake watatu, wameshindwa kufikishwa mahakamani hapo kama ilivyo kawaida leo Alhamisi, tarehe 5 Agosti 2021 na badala yake, kesi hiyo inasikilizwa kwa mtindo huo huku watuhumiwa hao wakiwa Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo ya uhujumu uchumi na kupanga njama za ugaidi inayosikilizwa na Hakimu Mwandamizi Hakimu Thomas Simba.

Jopo la mawakili watano wanaomtetea Mbowe na wenzake kwenye shauri hilo, wakiongozwa na Peter Kibatara, wameingia kwenye chumba maalumu kwenye mahakama hiyo majira ya saa 2:35 asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Ndani na nje ya viunga vya mahakama hiyo, ulinzi umeimalishwa ambapo tofauti na siku zingine, getini ili uweze kuingia ni lazima uonyeshe kitambulisho na kujibu baadhi ya maswali.

Magari ya polisi wenye silaha yameonekana yakizunguka maeneo mbalimbali ya mahakama yakiimalisha ulinzi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!