Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Kitimtim kortini, Hakimu ‘nitaita polisi’  
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Kitimtim kortini, Hakimu ‘nitaita polisi’  

Spread the love

MVUTANO umeibuka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kati ya upande wa Jamhuri na ule wa utetezi kwenye kesi ya uchochezi namba 112/2018 inayomuhusu Freeman Mbowe na wenzake wanane. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Kwenye kesi hiyo leo tarehe 22 Agosti 2019, mvutano huo umetokea na kuibua zogo n ahata kumsukuma Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba kutishia kuita polisi kutuliza ‘kelele’.

Kesi hiyo inamuhusi Mbowe, Mwenyekiyi wa Chadema Taifa, Dk.Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu -Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Shihidi wa saba wa Jamhuri Victoria Wihenge, ameieleza mahakama, kwenye uchaguzi wa marudi jimbo la Kinondoni, hakuna wakala wa chama chochote aliyezuiwa kwenye kituo cha kupiga kura.

Wihenge aliyejitambulisha kuwa ofisa wa uchaguzi katika Manispaa ya Kinondoni, ametoa ushahidi huo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya jana tarehe 21 Agosti 2019, kushindwa kuendelea kutokana na sababu ya afya yake kutokuwa imara.

Kwenye mahojiano yaliyofanyika leo, upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimbi; Dk. Zainab Mango; Wakili Wankyo na Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori

Upande wa utetezi umeongozwa na Prof. Abdallah Safari, Peter Kibatala, Dickson Matata, Hekima Mwasipu na Ekson Kilatu.

kabla ya kuibuka mvutano, Wakili Wankyo aliendelea kumuongoza shahidi huyo kuhusu ratiba ya uchaguzi kwenye jimbo la Kinondoni tarehe 21 Januari 2018 hadi tarehe 16 Februari 2018.

Ameeleza, tarehe ya kuchukua fomu iliyopangwa ni 14 Januari mpaka tarehe 20 Januari 2018. Wakili Wankyo amemuuliza idadi ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi ambapo amejibu vilikuwa 11.

Amevitja kuwa ni: AFP, CCK Demokrasia Makini, TLP, UPDP, DP, Chadema, CUF, CCM.

Wakili Wankyo alimuuliza kama anakumbuka wagombea wa uchaguzi huo. Hata hivyo, shahidi huyo amejibu anakumbuka wagombea wa vyama wawili ambao ni Maulid Mtulia (CCM) na Salim Mwalim (Chadema).

Amedai, kampeni zilianza tarehe 21 Januari 2018 na kumalizika tarehe 16 Februali 2018.

Na kwamba ipindi chote cha kampeni, wadau wote wa uchaguzi pamoja na wagombea “tulipaswa kuzingatia maadili ya uchaguzi rais, wabunge na madiwani.”

Utata ukaibuka

Wakati huo huo wakili Mwasipu, alikwenda kwenye kizimbani kwa ajili ya kuangalia kwenye meza ya shahidi kwa wasiwasi kuwa, kuna sehemu anasoma.

Kutokana na kitendo hicho, Wakili Wankyo alibuka na kulalamika kwa hakimu kwamba shahidi wao anatishwa.

Hakimu Simba aliingilia kati akisema, ataamuru askari wawakamate kwa kuleta vurugu mahakamani.

Kisha Wakili Kibatala aliinuka na kumlalamikia Hakim Simba kuwa wakili Nchimbi anambuguzi wakili Matata.

Peter Msigwa (mtuhumiwa) aliinuka na kudai “tunajisikia vibaya wakili wa serikali anavyowanyanyapaa mawakili wetu.”

Hakimu Simba alisema “hali imetulia, wameishaombana radhi kesi inaendelea.”

Shahidi ameendelea kueleza namna wasimamizi wa uchaguzi wanavyofuata taratibu na kanuni za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Shahidi ameeleza, vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi, wanavipa muongozo wa NEC kwa ajili kuwaongoza wakati wote wa kampeni na uchaguzi.

Amedai, muuongozo huo kutoka NEC ni kitabu au tangazo la serikali analopewa msimamizi wa uchaguzi na kuvipa vyama vya siasa.

Alipoulizwa kuhusu wajibu wa vyama vya siasa, ameeleza  “vyama vya siasa na wagombea kwa mujibu wa maadili ya uchaguzi, hawatakiwa kufanya kampeni zao wakiwa na namna yoyote ile ya kuashiria uvunjifu wa amani kama vile kutoa lugha za matusi.

“Pia kashfa, kejeli, udhalilishaji kwa walemavu , jinsia na kutumia lugha zitazohamasisha uvunjaji wa Amani, vurugu na kutoingia kwenye vituo vya kupiga kura kwa nguvu au lazima.”

Shahidi huyo ameeleza, “maadili yanatutaka sisi wote kwa pamoja watumishi wa serikali na wagombea kutokuwa na matumizi ya simu ndani ya kituo cha uchaguzi.”

Alipoulizwa kuhusu mambo yanayokatazwa wakati wa kampeni, ameeleza “tunakatazwa kutumia mikutano ya kampeni kama sehemu ya uvunjifu wa amani pamoja ubebaji wa silaha za jadi na za moto na matumizi yake, lugha za vitisho hazitakiwi.”

Ameeleza, kampeni zinatakiwa kunadi sera za chama husika ili kuwahamasisha kumpigia kura.

Utata waibuka tena

Utata umeibuka wakati Wakili Kibatala alipoinuka na kudai, kuwa shahidi ana simu kwa kuwa anaonekana kuna sehemu anasoma.

Hakimu alimuita askari ili kwenda kuangalia kwenye kizimba cha shahidi kama kuna kitu anasoma …”leo mmekula nini,” alihoji hakimu.

Baada ya askari kwenda kuangalia, Hakimu Simba alimwamuru kuendelea kutoa ushahidi.

Wakili Wankyo alimuuliza shahidi kuhusu sheria ya uchaguzi, shahidi alieleza kuwa msimamizi wa uchaguzi anatakiwa kuvitaarifu vyama vya siasa kuwasilisha majina ya mawakala ikiambatana na orodha ya vituo vya kupigia kura siku saba kabla ya uchaguzi.

“Msimamizi wa uchaguzi aliandika barua kama inavyotakiwa kwa vyama 11,…vyama viliwasilisha majina ya mawakala na baadaye likafuata zoezi la uapishaji wa mawakala,” ameeleza.

Amedai, tarehe 10 Februari 2018 mawakala wa vyama vya AFP, CCM, CCK, CUF, UMD DP, TLP, Chadema, Demokarasia Makini waliapishwa.

Na kwamba baada ya mawakala kuapisha kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, zoezi lilifuata ni msimamizi wa uchaguzi kuwatambulisha mawakala kwa wasimamizi wa vituo.

Ameeleza, “mheshimiwa hakimu, msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa ya Kinondoni, aliandika barua ya kuwatambulisha mawakala kwa wasimamizi wa vituo… aliwatambulisha tarehe 17 Februari 2018 asubuhi kabla ya kuanza kupiga kura.”

Mahojiano yalikuwa hivi…

Wakili Wankyo: Mawakala walitambulikaje tarehe 17 Februali?

Shahidi: Mawakala walipaswa kufika kwenye vituo wakiwa na vitambulisho vyao.

Wakili Wankyo: Vitambulisha vya aina gani?

Shahidi: Kinaweza kuwa kitambulishao cha benki ya taifa, au hata kadi ya bima ya afya au kitambulisho cha kupiga kura.

Wakili Wankyo: Baada ya mawakala kwenda kwenye vituo vya kupiga kura, ni vitu gani wanavyopaswa kuwafanya?

Sahidi: Baada ya kufika, mawakala wataonesha vitambulisho vyao ili kuweza kuwatambua.

Wakili Wankyo: Atawatambuaje?

Shahidi: kwa kutaja jina na kuonesha kitambulisho pamoja barua .

Wakili Wankyo: Ni mambo gani ya muhimu ya muhimu ulifanya ili watu wanaohusika kupata taarifa hiyo ya utaratibu wa mawakala?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, uchaguzi ni Process (hatua kwa hatua)…

Hakimu: jibu swali uliloulizwa.

Shahidi: Tulikaa kikao kwa ajili ya kujadili suala hilo.

Wakili Wankyo: Mwambie hakimu hiko kikao mlikaa na nani?

Shahidi: Vyama vyote vilivyotoa wagombea.

Wakili Wankyo: Vitaje angalai kwa uchache?

Shahidi: Alikuwepo mjumbe CCK, AFP, CCM UMD, Demokrasia Makini, Chadema, TLP.

Wakili Wankyo: kama unakumbuka, ilikuwa tarehe ngapi?

Shahidi: Tarehe 30 mwezi wa kwanza 2018.

Wakili Wankyo: ajenda za kikao hiko zilikuwaje?

Shahidi: Kikao kilikuwa na ajenda ya uwapishaji mawakala na utaratibu wa uchaguzi.

Wakili Wankyo: Iambie mahakama sasa, makubaliano yalikuwa ni yapi?

Shahidi: Kuwatambulisha mawakala kwenye vituo kwa barua.

Wakili Wankyo: Kutoka kwa nani na kwenda kwa nani?

Sahidi: Kwa Msimamizi wa uchaguzi wa Kinondoni kwenda kwa wasimamizi wasaidizi wa kata na mitaa.

Wakili Wankyo: ifafanulie endapo katika vyama vya 11 akajitokeza mwakilishi kuja kufuatilia barua za kuwatambulisha mawakala, wewe kama ofisa uchaguzi.

Shahidi: kimya.

Wakili Wankyo: Nataka uiambie mahakama tarehe 16 kama kuna mtu yoyote aliyedai barua?

Shahidi : Hakuna chama kilichojitokeza kudai barua bali vilidai kiapo.

Hakimu: Kiapo gani?

Shahidi: Kiapo cha kutunza siri.

Hakimu: Endelea.

Shahidi: Kwa madai kwamba kitawatambulisha kwenye vituo vya kupiga kura.

Wakili Wankyo: Ifafanue mahakama hiko kiapo kilikuwa cha aina gani?

Shahidi: Mheshimiwa hakimu, kwa mujibu wa sheria ya tume ya uchaguzi, fomu namba sita ambapo mla kiapo (wakala) anatoa mbele ya msimamizi wa uchaguzi kwa kutunza siri zote atakazoziona na kuzijua ndani ya kituo cha kupiga kuta.

Wakili Wankyo: Kwenye hiyo fomu namba sita, anaapaje?

Shahidi: Mla kiapo atajaza fomu namba sita, ataapishwa na ataweka saini yake, mwapishaji atamalizia kwa kuweka saini yake na muhuri, kiapo hiko kitahifadhiwa na mla kiapo.

Wakili Wankyo: Ifahamishe mahakama katika eneo hilo kwa kipindi cha uchaguzi, nini matumizi ya kiapo hicho?

Shahidi: Kiapo hiko ni kwa ajili ya matumizi ya ofisi endapo mla kiapo atakiuka masharti ya kiapo hiko.

Wakili Wankyo: Ni wakati gani kiapo hicho kinakabidhiwa kwa muapaji?

Sahidi: Mheshimiwa hakimu, hakuna wakati muapaji anakabidhiwa kiapo hiki.

Wakili Wankyo: Kiapo hiki kinaenda wapi?

Hakimu: unarudia mara ya pili ushauliza hilo.

Wakili Wankyo: Kiapo hiko kinaweza kumtambulisha wakala?

Shahidi: Hakuna kiapo kitachoweza kumtambulisha wakala zaidi ya barua.

Wakili Wankyo: ulidai kuna chama kilikija kudai kiapo ni chama gani na ulilishughulikiaje?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu kiapo kilikuja kudaiwa na Chama cha Demokrasia Chadema.
“Tarehe 16 walifika viongozi wa Chadema kwenye ofisi ya msimamizi wakiomba tuwapatie kiapo cha mawakala.”

Wakili Wankyo: Ni wakati gani?

Shahidi: Mchana.

Wakili Wankyo: Walikuja viongozi gani ?

Shahidi: alikuja Mbunge wa Viti Maalum, Suzani Limo na Mheshimiwa Ester (Ester Matiko) wa Mkoa wa Mara.

Wakili Wankyo:  Pamoja na nani unayemkumbuka?

Shahidi: Ninawakumbuka wawili lakini walikuja watatu.

Wakili Wankyo:  Hao ambao umewataja kwa mara ya kwanza uliwafahamu lini?

Shahidi: Mheshimiwa Lyimo tulikuwa naye kwenye Baraza la Madiwani na Ester Matiko ndio nilimuona siku hiyo.

Wakili Wankyo:  Ulijuaje kama huyo ni Ester Matiko?

Shahidi: Walijitambulisha.

Wakili Wankyo:  Ifahamishe mahakama walijitambulishaje?

Shahidi: Msheshimiwa Hakimu walijitambulisha kuwa wanatoka Chadema na wamefuatilia viapo vya mawakala.

Wakili Wankyo:  Iambie mahamama, uliishughulikiaje shida yao baada ya kujitambulisha?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, tuliwaambia kiapo sio kitambulisho cha wakala bali kuna barua inayoandikwa na msimamizi wa uchaguzi.
“Kuhusu kiapo tuliwaeleza namna msimamizi anavyokitumia kwenye uchaguzi”

Wakili Wankyo: Iambie mahakama, muitikio ulikuaje mara baada ya kuwaeleza hawa Ester Matiko na Suzani Lyimo?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, wote walikubaliana na msimamizi wa uchaguzi wakaondoka.

Wakili Wankyo:  Walikwenda wapi?

Shahidi: Sikuweza kujua

Wakili Wankyo:  Watu hao unaweza kuwatambua?

Shahidi: Naweza nikajaribu.

Wakili Wankyo:  Kama unakumbuka, mwambie hakimu umewaona?

Shahidi: Kimya.

Prof. Safari akaingilia kati: Mheshimiwa hii ya kujaribu sio sawa.

Hakimu: Yes, ukimwambia ajaribu akikosea…endelea.

Shahidi: kutoka Januari hadi leo ni muda mrefu siwezi kukumbuka.

Wakili Wankyo: Nini kiliendelea baada ya hao kuondoka ukiwa kwenye utekelezaji wa majukumu yako?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi iliendelea na maandalizi ya uchaguzi uliofanyika kesho yake.

Wakili Wankyo:  Zoezi la barua za mawakala lilifanyika lini?

Shahidi: Tarehe 17.

Hakimu: Tarehe 17 mwezi gani mwaka gani?

Shahidi: mwezi wa pili mwaka 2018.

Wakili Wankyo:  Kuna chama chochote kilichopata barua ya uwakala kabla ya tarehe hiyo?

Shahidi: Hakuna.

Wakili Wankyo:  kwanini?

Shahidi: Kwa mujibu wa taratibu za tume.

Wakili Wankyo:  Uchaguzi ulifanyika lini?

Shahidi: Tarehe 17 Februali 2018.

Wakili Wankyo:  Ni vyama gani vilivyoshiriki uchaguzi huo?

Shahidi: Mheshimiwa hakimi vyama 11.

Wakili Wankyo:  Ulisema vyama gani?

Hakimu: Nilisharekodi.

Nchimbi: Mheshimiwa hakimu shahidi anasisitiza kilichotokea tarehe 17.

Hakimu : vyama gani?

Shahidi: CCK. UMD, DP, Demokrasia makini , Chadema.

Wakili Wankyo:  Walau kwa ufafanuzi, ni chama gani kilicholeta malalamiko kwa maana mawakala hawakupewa barua ya kutambulika au hawakuapishwa?

Shahidi: Chama cha Mapinduzi ndio kilileta lalamiko.

Wakili Wankyo:  kwa tarehe hiyo, chama chochote kilicholeta lalamiko la kuzuiliwa kwa wakala wao kwa kukosa barua?
Shahidi: Hakuna wakala aliyezuiliwa.

Wakili Ankyo amemaliza na kumkabidhi kijiti Wakili Nchimbi kuendelea kumuongoza shahidi wa Jamhuri

Wakili Nchimbi: shahidi uliongolea katazo la kampeni na siku ya uchaguzi na ukasema ni kwa mujibu wa maadili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani na ukasema kuwa ni tangazo la serikali, iambie mahakama tangazo hilo namba ngapi?

Shahidi: 254 la mwaka 2015.

Wakili Nchimbi:  Uiambie mahakama, haya maadili ya uchaguzi yanatumika kwa kipindi kipi na kwa chaguzi zipi?

Shahidi: kwa miaka mitano kwa maana kuanzi 2015 mpaka 2020.

Wakili Nchimbi:  Uliiambia mahakama kwamba, maadili haya ni makubaliano kati ya nani na nani?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, ni makubaliano kati ya vyama vya siasa, serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakili Nchimbi:  Makubaliano katika jambo lipi hasa?

Wakili Nchimbi:  Kwenye uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.

Wakili Nchimbi:  Labda ukiifahamisha mahakama hii, ungetufahamisha makubaliano hayo ikitokea chama cha siasa au wafuasi wake wakikiuka, kuna nini cha kuwajibisha?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, kukiuka kwa maadili hayo sheria itafuata mkondo wake

Wakili Nchimbi:  Kwa nafasi yako hatua gani itachukuliwa?

Shahidi: kamati ya maadili itaitana.

Wakili Nchimbi:  Nini kitachukuliwa?

Shahidi: Kamati ya Maadili itasimamisha kampeni ya chama husika.

Wakili Nchimbi:  kusimamisha kampeni au?

Shahidi: kupewa onyo au kuondolewa katika uchaguzi.

Wakili Nchimbi:  Utaielezeaje mahakama kuhusiana na kampeni ya chama chochote cha siasa ambacho kinamgombea kikakiuka maadili?

Shahidi: mkutano huo utazuiliwa.

Wakili Nchimbi:  kwa sababu gani?

Shahidi: kwa sababu ya kukiuka maadili

Wakili Nchimbi:  wanaohusika na uzuiaji huo ni kina nani?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, polisi wanaweza kuzuia au msimamizi wa uchaguzi.

Nchimbi: Ni wakati gani msimamizi wa uchaguzi ataweza kusimamisha mkutano wa aina hiyo?

Shahidi: Katika kikao cha maadili

Wakili Nchimbi:  kwa hiyo baada ya kikao cha maadili kupita, malalamiko

Shahidi: ndio.

Wakili Nchimbi:  hili kaishalisema na kaweka sawa.
(kicheko mahakama mzima).

Wakili Nchimbi:  kwa kumaliza kama unakumbuku mkataba wa serikali na msimamizi ni vyama gano viongozi wao waliweka saini?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, nakumbula makatibu wakuu ndio waliosaini

Wakili Nchimbi:  ni wa vyama gani

Shahidi: ACT, CCK, CCM, Chadema, Demokrasia Makini, TLP, DP, UMD, Ada Tadea, DM.

Upande wa Jamhuri umemaliza kumuongoza shahidi.

   Itaendelea……….

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!